Bibi wa miaka 69 mkazi wa Katabe wilaya ya Rungwe aitwaye Aida Mwangosi ameuawa kwa kukatwa na kitu chenye ncha kali kichwani na usoni na mtu au watu wasiofahamika akiwa nyumbani kwake.
Tukio hilo limetokea jana majira ya saa 7:30 mchana huko katika kijiji cha Katabe, kata ya Kyimo, tarafa ya Ukukwe wilaya ya Rungwe mkoa wa Mbeya. Aidha katika tukio hilo Hawa George (12) mwanafunzi shule ya msingi Katabe darasa la pili ambaye ni mjukuu wa marehemu alijeruhiwa kwa kukatwa kitu chenye ncha kali kichwani kisha kubakwa na amelazwa hospitali ya Makandana-Tukuyu.
Chanzo cha tukio kinachunguzwa, ndani ya nyumba ya marehemu kumekutwa shoka na jiwe moja kubwa ambavyo vinadhaniwa kutumika katika tukio hilo. Uchunguzi zaidi wa tukio hili unaendelea.
Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya kamishina msaidizi mwandamizi wa polisi Ahmed Msangi anatoa wito kwa jamii kutowaacha wajane na wazee wenye umri mkubwa na watoto wadogo bila uangalizi wa karibu ili kuepusha watu wenye nia mbaya au wahalifu kutopata nafasi ya kutekeleza uhalifu wao.

Aidha anatoa wito kwa yeyote mwenye taarifa za mtu au watu waliohusika na tukio hili azitoe katika mamlaka husika ili akamatwe au wakamatwe na hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yao.

0 comments:
Chapisha Maoni