KWA mara nyingine, staa wa sinema za Kibongo, Yobnesh Yusuf ‘Batuli’
amemwaga data za kimapenzi akidai hajawahi kumpenda mwanaume kama
alivyompenda Nice Mohammed ‘Mtunis’.
Batuli alisema licha ya
kuwa walimwagana na staa huyo lakini hatokuja kupenda mwanaume kama
alivyompenda Mtunis.
Nilivyompenda Mtunis ni ngumu sana kumpenda mwanaume mwingine kama hivyo na kwa kawaida kupenda huwa ni mara moja tu mengine tutadanganyana
alisema Batuli.
Hivi karibuni Batuli aliripotiwa kutikisa ndoa ya Mtunis ikidaiwa
kuwa bado ana uhusiano naye lakini cha ajabu mtoto wa kike hakuonesha
dalili zozote za kukanusha taarifa hizo.
0 comments:
Chapisha Maoni