
Jeshi la polisi mkoa wa Mbeya linamshikilia mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Biton Martin (25) mkazi wa kiwira akiwa na miche miwili ya bhangi nyumbani kwake.
Mtuhumiwa huo alikamatwa katika mtaa wa Kiwira Road, kata ya Kawetele, tarafa ya Tukuyu, wilaya ya Rungwe, mkoa wa Mbeya jana majira ya saa 18:30 jioni. Mtuhumiwa ni mkulima wa zao hilo haramu na taratibu za kumfikisha mahakamani zinafanywa.



0 comments:
Chapisha Maoni