Alhamisi, Mei 08, 2014

JESHI LA POLISI MBEYA LINAMSHIKILIA RAIA WA ETHIOPIA KWA KUINGIA NCHINI KINYEMELA


Jeshi la polisi mkoa wa Mbeya linamshikilia raia na mkazi wa nchini Ethiopia aitwaye Damisye Abid (40) akiwa ameingia nchini bila kibali.
Mtuhumiwa alikamatwa katika msako ulioendeshwa jana majira ya saa 06:30 asubuhi huko katika mtaa wa stendi kuu kata na tarafa ya Sisimba, jiji na mkoa wa Mbeya, taratibu za kumkabidhi idara ya uhamiaji kwa hatua zaidi za kisheria zinaendelea.

0 comments:

Chapisha Maoni