Nguli wa filamu za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ ameziomba mamlaka
zinazosimamia maadili ya filamu nchini ziwaruhusu wasanii waigize nusu
utupu ili kuendana na soko la kimataifa.
Akitetea wakati akizungumza na chanzo chetu cha habari, staa huyo aliyeitendea
haki filamu ya Foolish Age alitolea mfano Tamthiliya ya Shuga iliyomtoa
Lupita Nyong’o ambayo alicheza akiwa nusu utupu.
Wanasema hatufuati maadili wakati kuna muvi ambazo zipo theatre na watu wanaangalia hazina maadili, wao wanataka tufanye vitu kwa kudanganya wakati sasa hivi tuko dunia ambayo tuna takiwa tuweke vitu wazi, wasibane sana
alisema Lulu.




0 comments:
Chapisha Maoni