Wakati mjadala kuhusu sura ya kwanza na sita kwenye Bunge Maalumu ukielekea ukingoni, baadhi ya wajumbe wametoleana kauli ambazo zimesababisha kutoelewana.
Kiini cha hayo ni aina ya muundo wa Muungano unaotakiwa kuwekwa kwenye Katiba Mpya, suala ambalo wajumbe badala ya kulijadili kwa hoja, wakaishia kushambuliana kwa maneno.

Kwa muda mrefu hali haikuwa shwari, kwani dakika 10 zilizotengwa kwa ajili ya mjumbe kuchangia mjadala, wengi walizitumia kumaliza hasira dhidi ya wenzao au kuponda mchango uliotolewa awali na mjumbe mwingine.
Hebu tuone mifano ya kauli zilizoacha majeraha bungeni hivi karibuni.
Kauli ya Lukuvi
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu - Sera Uratibu na Bunge, William Lukuvi alisema Chama cha Wananchi (CUF) ni sehemu ya kikundi cha Uamsho kinachoisumbua Serikali ya Zanzibar.
Lukuvi akaenda mbali zaidi na kusema Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharifu Hamad, ni mchochezi ambaye amemtuhumu Rais Jakaya Kikwete kuvuruga Muungano na kudai anastahili kupelekwa katika Mahakama ya Uhalifu wa Makosa ya Jinai The Hague - Uholanzi.
Kauli hii inaweza kuonekana kama njia ya kuzuia wananchi wasikiamini Chama cha CUF katika mchakato wa Katiba Mpya.
Profesa Ibrahim Lipumba
Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba akihitimisha hotuba kwa mujibu wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), akalifananisha Bunge Maalumu na kundi la Intarahamwe.
Kundi hilo ni lile lililoendesha mauaji ya kimbari nchini Rwanda, mwaka 1994.
Felix Mkosamali
Mbunge wa Muhambwe, Felix Mkosamali alisema Rais Jakaya Kikwete na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, Anne Makinda, ni viongozi vigeugeu ambao hawawezi kufikisha nchi mahali popote.
Kiumri Mkosamali ni mdogo kuliko wabunge wote wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Alisema nchi haiwezi kuendelea kuongozwa na viongozi vigeugeu, kauli ambayo imewachukiza zaidi viongozi wa Serikali.
Vijembe kutoka Zanzibar
Mwakilishi wa Mji Mkongwe, Ismail Jussa alieleza kuwa baadhi ya wajumbe wenzake kutoka Zanzibar ‘wameufyata’, akimaanisha hawakutetea walichokubaliana kabla ya kufika Dodoma.
Hata hivyo, naye akapigwa kombora na Asha Bakari Makame, ambaye alitafsiri kuufyata kuwa ni sawa na mtu mwenye busha.
Akaeleza bungeni kuwa mwenendo wa maisha ya Jussa unatia shaka kwa sababu ana umri mkubwa, lakini hajaoa wala hana watoto.
Masauni na Kupindua Serikali
Hamad Masauni Yussuf alituhumu wanaopinga Serikali mbili kuwa ndiyo wamekuwa na mbio za kutaka kupindua Serikali.
Pia alisema kauli za wajumbe hao zinaifafanisha hati ya Muungano na barua ya mapenzi, akaeleza bungeni kuwa watakaporejea Zanzibar watawahangaikia watu hao hata kama watajificha shimoni.
Omary Ali Shehe
Huyu naye akaibuka na kauli tata akisema, “Wanaolazimisha serikali mbili mpaka kutokwa povu mdomoni ni wanafiki na wasaka tonge.”
Mrema na Sanya
Mbunge wa Vunjo, Augustino Mrema alishauri watu wasikubaliane na Serikali tatu kwa sababu hali ya usalama ya taifa siyo shwari, hasa kwa Zanzibar aliyodai inanyemelewa.
Mohammad Sanya
Mkongwe huyu wa siasa za upinzani Zanzibar akaita wawekezaji kutoka Tanzania Bara waliopo visiwani humo kuwa ni wauza karanga na dawa za mende. Alitaka Zanzibar iachwe ijijenge kwa kiwango cha kuwa Dubai na Hong Kong nyingine.
Diana Chilolo
Anasema ana shaka juu ya Tundu Lissu kufunga ndoa na wajumbe kutoka Zanzibar na kwamba anashangaa ndoa hiyo ni ya aina gani.
Lissu na Askofu
Tundu Lissu alisema kukosoa yaliyofanywa na Hayati Mwalimu Julius Nyerere, siyo dhambi kwa kuwa hakuwa Malaika wala Mungu hivyo alipokosea lazima akosolewe hadharani.

0 comments:
Chapisha Maoni