Leo ni Jumatatu tarehe 21 Mfunguo Tisa Jamadil Thani mwaka 1435 Hijiria, inayosadifiana na Aprili 21 mwaka 2014 Miladia.
Siku kama ya leo miaka 76 iliyopita, Allamah Muhammad Iqbal Lahore mwanafikra, mwanafalsafa na malenga wa Kiislamu aliaga dunia huko Bara Hindi. Alizaliwa mwaka 1873 katika mji wa Sialkot kwenye jimbo la Punjab. Baada ya kumaliza masomo ya awali na ya juu na kupata shahada ya uzamili Allamah Muhammad Iqbal Lahore alielekea nchini Ujerumani na baadaye Uingereza kwa lengo la kujiendeleza katika elimu ya falsafa na kubaki huko kwa kipindi cha miaka minne. Malenga huyo alianza kutunga mashairi tangu akiwa katika masomo yake ya sekondari ya juu. Baada ya kurejea India, Iqbal Lahore alianza kuwaamsha Waislamu wa nchi hiyo na kufanya jitihada za kuwaunganisha pamoja huku akibainisha fikra na mitazamo yake kupitia beti za mashairi. Mwanafalsafa huyo anahesabiwa kuwa mmoja wa waanzilishi na waasisi wa Pakistan huru.
Miaka 1185 iliyopita, Egbert Mfalme wa kwanza wa Uingereza aliingia madarakani baada ya vita vya muda mrefu. Kabla ya hapo Uingereza ilikuwa ikiendeshwa kwa utawala wa kijadi na ilikuwa imegawanywa katika sehemu kadhaa huku kila mtawala akitawala eneo lake. Egbert alikuwa mfalme wa ardhi ya Wessex na baada ya kupigana vita na watawala wa kijadi na kuwalazimisha wamtii, aliingia madarakani akiwa Mfalme wa Kwanza wa Uingereza na kuasisi mlolongo wa utawala wa Wasaxoni. Mtawala huyo alijulikana pia kwa jina la Egbert the Saxon.
Na miaka 34 iliyopita aliaga dunia Sohrab Sepehri malenga na mchoraji mashuhuri wa Kiirani. Sohrab alizaliwa mwaka 1307 Hijria Shamsiya katika mji wa Kashan katikati mwa Iran. Awali malenga huyo wa Kiirani alianza kufundisha na baada ya hapo alijiunga na fani ya sanaa. Aidha alikuwa na kipawa kikubwa katika masuala ya uchoraji. Kazi za malenga na mchoraji huyo wa Kiirani zilimpatia tuzo na zawadi nyingi katika maonyesho mbalimbali yaliyofanyika ndani na nje ya Iran. Shairi lake la kwanza alilitunga mwaka 1330 Hijria Shamsiya na kulipa jina la Marge Rang au The Death of Colours kwa kimombo.

0 comments:
Chapisha Maoni