Mkutano wa umoja wa katiba ya wananchi-Ukawa- uliozuiliwa na jeshi la polisi mara mbili umefanyika leo katika uwanja wa Kibandamaiti mjini Zanzibar huku viongozi wakuu wa vyama vitano vya upinzani wakihudhuria na kuhutubia.
Mkutano huo ulihudhuriwa na mamia ya wanachama,wapenzi na waanchi kwa mara ya kwanza kushuhudia mkutano wa kisiasa ukihutuiwa na viongozi wakuunamaktibu wa vyama vitano vikuu vya upinzani ambapo katibu mkuu wa chamacha waanchi cuf maalim seif sharrif hamadi ambaye alikuwa mwenyeji wa mkutano huo alitamka kuinga mkono ukawa wa kwanza kuanika nguvu zake za kudai serikali tatu alikuwa mwenyekiti wa chama cha NLD mhe Emamanuel Makaidi ambaye alisema tanganyika lazima ipatikane
Na ndipo wakafuatiwa na wenyeviti wa NCCR Mageuzi James Mbatia ambaye alifafanua kuhusu rasimu hiyo na utaratibu wake huku mwneyekiti wa CHADEMA mhe Freeman Mbowe kwa upandewake ametangaza rasmi kwa kuwa umoja mpya wa vyama vyasiasa kuleljkeauchaguzimkuu ,na mwisho alikuwa mwenyekiti wa CUF professa Ibarim Lipumba ambayealiichanua rasimu hiyo na kuwapinga wanaiopigia debe serikali mbili.
Huu nimkutano mkubwa na wa kwanza kufanyika Zanzibar kuhusu rasimu na bungelake ambapo umoja huo sasa unaelekea kisiwani Pemba kwa kazi hiyo.

JUSA
Jussa alipanda kuwakilisha wabunge wote wa UKAWA kutokea Zanzibar. Amewaambia Wazanzibar wawe tayari kuwasaliti na kuwazomea wale wote wanafiki wanaowasaliti wanapofika Dodoma kama Asha Bakari.
Amesema Wazanzibar wawashukuru watu kama akina Freeman Mbowe, James Mbatia, Tundu Lissu, John Mnyika na UKAWA nzima kwa kuwa wamesimama kidete kuitetea Zanzibar tofauti na Wazanzibar wengine kama akina Asha Bakari, Balozi Seif Idd na wawakilishi wote wa CCM kutoka Zanzibar.
Amemtangaza Balozi Seif Idd kuwa adui namba moja wa Zanzibar kwa ububu wake bungeni kama kiongozi mkuu kutoka Zanzibar ndani ya Bunge Maalum la Katiba.
Akaongeza kusema ujanja ujanja wanaotaka kufanya wa kubadilisha sheria ya mabadiliko ya katiba kuondoa sharti la 2/3 anasema wafanye wafanyavyo lakini hawataweza kwa kuwa mtarimbo umeganda.
Jussa akasema yeye alikuwa anaweza uwanja sawa tu lakini mchezaji hasa ni anayekuja punde ambaye ni Tundu Lisu.

TUNDU LISSU
Wazanzibar wanamwita Lissu Christiano Ronaldo. Wananchi wameshangilia balaa alipoanza kwa kuwasalimia kwa jina la Zanzibar Huru na Tanganyika Huru na Shirikisho lenye hadhi kuu ya nchi.
Kwa miaka 50, anasema Tundu Lisu, Zanzibar imekuwa koloni la Tanganyika, Zanzibar imefungwa minyororo na Tanganyika na sio huru tena.
Kwa miaka 50 masuala yote ya nje yamekuwa yakiamriwa Dar es Salaam, Mambo ya Ulinzi yanaamriwa na Dar, masuala ya fedha ya Zanzibar yamekuwa yakifanywa na Dar na kwa hiyo ni koloni la Tanganyika.
Anasema mtia minyororo kwa mtu mwingine naye pia hawezi kuwa huru. Akatolea mfano wa mfunga minyororo wa magereza kuwa naye hawezi kuondoka., hivyo Tanganyika iliyoifunga Minyororo Zanzibar nayo haiko huru.
Akasema Tanganyika ilikana jina lake na kuliondoa kwenye katiba ili iendelee kuinyonya Zanzibar, anasema ilikuwa na Tanganyika huru ni kuwa na Zanzibar huru.
Amkaribisha sasa Maalim Seif;
MAALIM SEIF
Maalim Seif jukwaani sasa; kaanza kwa kumtambulisha Mzee Moyo ambaye alikuwa Waziri wa Katiba wa Mzee Abeid Amani Karume, Mzee Moyo kasema 'ni tatu, tatu, tatu bila mzaha'. Kasema leo anaacha majembe yazungumze.
Maalim amesema kama wanaogopa Shirikisho la Serikali Tatu, basi yeye yuko tayari kuunga mkono serikali mbili kwa maana ya Zanzibar huru na Tanganyika huru, tofauti na hapo kila mtu na lwake.
Maalim anawatambulisha viongozi wa UKAWA nje ya bunge, akianza na Mosena Nyambabe- Katibu Mkuu wa NCCR Mageuzi.
Maalim Seif akaongeza kusema kuwa kama Kikwete anao uwezo wa kuwadhibiti Wazanzibar basi aende na cha moto kitaonekana.
Amesema kuwa kuna magari yameletwa kwenye mkutano na vikosi vya KMKM, akaasa kuwa ole wake aguswe mtu akasema anazungumza kama Makamu wa Rais, watajua jini liliko Zanzibar, uwanja ukalipuka kwa shangwe na nderemo.
Akapanda Emmanuel Makaidi mzee wa 'Moto moto motoooo...uwachome CCM'...

MAKAIDI
Makaidi amesema kuwa Watanganyika wamebakia bila serikali kwa sababu Mwalimu Nyerere Baba wa Taifa aliitupa serikali yote ya Tanganyika kwenye Muungano na Karume hakuitupa yote na ndiyo maana wamekuwa ngaringari leo.
Amewaomba Wazanzibar kuungana na Watanganyika kudai serikali zao...
Makaidi anasema CCM hakuna wanasiasa bali wajasiriamali na ndiyo maana hawataki kujisahihisha kama Mwalimu alivyotaka. Kisha akapanda Mtikila...
DKT. SLAA
Dkt. Slaa amesema kuwa Jeshi la Tanzania halijakosa uzalendo kama walio nao mafisadi wa CCM na serikali yake. Kutokana na uzalendo ambalo JWTZ linao kwa wananchi na nchi, haliwezi kupindua serikali eti tu kwa sababu ni Shirikisho la Serikali Tatu.
Anasema kuwa wanajeshi wetu wamekuwa wazalendo kiasi cha kuvumilia kukosa mishahara, maslahi yao madogo na shida nyingine iweje wafanye hivyo kwa serikali tatu, amesema Kikwete halijui jeshi ndiyo maana amepotoka...
Maalimu Seif aliendelea ambapo aliwasihi viongozi wa UKAWA kujiimarisha na kuulinda UKAWA kwani wabaya wao wanajipanga.
Akasema kuwa wakati wa kutishana tishana umeshapita. Kuendelea kutisha Wazanzibar ni kuwaongezea ari na hamasa.
MTIKILA
Mtikila; Kinachowasumbua CCM kuhusu serikali tatu ni unywani. Watanganyika wanapumbazwa kuwa uhuru ni mizinga uwanja wa taifa. Anasema kuwa kuwatisha wananchi na majeshi ni ugonjwa wa apedomia. Wanasahau kuwa wanajeshi wana ndugu zao wengi uraiani. Akamalizia kwa kusema saa ya ukombozi ni sasa...
MBATIA
Mbatia; muungano haukuridhiwa kwa sheria za Zanzibar kwa hiyo ni batili. Anasema Zanzibar kujitangazia mamlaka yake ni kuikomboa Tanganyika. Amesema kuwa wajumbe wa UKAWA kutoka Zanzibar wamewanyima turufu majiCCM huko BMK hivyo asitokee mtu wa kuisaliti Zanzibar.
Amesema kuwa chokochoko za udini zinapandikizwa na CCM, lakini hazitafua dafu. Anasema huwezi kuwa muislamu safi halafu ukahubiri udini na ubaguzi wa aina yoyote, huwezi kuwa Muislam safi kisha ukahubiri matusi na kejeli. Vivyo hivyo kwa mkristo safi.
MBOWE
Mbowe; maandamano nchi nzima ya kudai Katiba Mpya na bora inayotokana na maoni ya wananchi yanakuja baada ya mikutano ya Zanzibar. UKAWA haitarudi bungeni kushiriki dhambi ya kupingana na maoni ya wananchi, dhambi ya kuhubiri matusi kwa wananchi.
Amesema kuwa UKAWA huu si kwa ajili ya Katiba tu bali ni kwa ajili ya maslahi halisi ya wananchi. Ametangaza rasmi kuvunja Baraza Kivuli na sasa ataliunda upya kwa ushirika na NCCR, CUF CHADEMA.
Wananchi wamelipuka kwa furaha baada ya Kamanda Mbowe kutangaza kuwa UKAWA utaendelea hadi uchaguzi.

PROF LIPUMBA
Prof. Lipumba; wanaopinga serikali tatu kwa kigezo cha gharama hawajielewi. Anasema nchi inaingizwa kuzimu kwa matumizi ya hovyo na mabovu ya serikali kila siku.
0 comments:
Chapisha Maoni