STAA wa filamu na mduara Bongo, Zuwena Mohamed ‘Shishi
Baby’ amefunguka kuwa amenasa vilivyo katika penzi la msanii mwenzake,
Nuhu Mziwanda hatarajii kuachika.
Staa wa filamu na mduara Bongo, Zuwena Mohamed ‘Shishi Baby’ akiwa kwenye pozi la kimahaba na mpenzi wake aliyefahamika kwa jina la Nuhu Mziwanda. |
Akipiga stori na paparazi wetu, Shishi alisema yupo tayari kuolewa na
Mziwanda kwani anampenda na ndiyo ubavu wake kutokana na vile ambavyo
amekuwa akimwonesha mapenzi ya kweli tofauti na wapenzi wake wote
waliopita.
“Huyu ndiye shemeji yenu, ndiye mume wangu mtarajiwa, ninampenda na yeye
ananipenda kwa hiyo Mungu akijalia soon tutakamilisha taratibu za
ndoa,’’ alisema Shishi Baby.
0 comments:
Chapisha Maoni