Jumatano, Aprili 16, 2014

BABY MADAHA ADAI ATAOLEWA 2030

STAA wa muziki na filamu Bongo, Baby Madaha amesema hana papara na suala la ndoa kwani amejipanga kutimiza tendo hilo mwaka 2030.
Akizungumza na paparazi wetu, Baby alisema anachoomba ni uzima kwani suala la ndoa analiona halina umuhimu kwa sasa kwani ni kipindi cha yeye kusaka fedha kwa hali na mali.
“Sina haraka bwana, maisha haya yanahitaji kuyatengeneza, najipanga Mungu akipenda labda kwenye 2030 huko ndiyo nitafunga ndoa sasa hivi acha nitengeneze chapaa,” alisema Baby ambaye umri wake unakadiriwa kutopungua miaka 30.

0 comments:

Chapisha Maoni