Mlinda mlango wa Chelsea,Petr Cech amehoji kama Liverpool wanaweza kuhimili presha ya mbio za ubingwa.
Liverpool wapo kileleni kwa tofauti ya pointi mbili katika msimamo wa
ligi kuu ya Uingereza mara baada ya kupata ushindi muhimu wa goli 3-2
dhidi ya Manchester City pale Anfield.
Ushindi wa michezo kumi mfululizo umefanya kikosi cha Brendan Rodgers
kuwaacha nyuma wapinzani wao huku ikiwa imebaki michezo minne na kuwa
na matumaini makubwa ya kupata taji la kwanza tangu mwaka 1990.
Lakini moja ya michezo hiyo ni dhidi ya Chelsea katika uwanja wa
Anfield,Aprili 27 na Cech anasubiri kuona kama Liverpool wanaweza
kuendeleza kiwango chao bora na kuweza kumaliza wakiwa vinara mpaka
mwisho.
Huku akisema,”Hakuna mtu aliyetarajia chochote kutoka kwa Liverpool
na kwasasa wapo katika kiwango imara na hiyo ni kwasababu wanacheza bila
aina yeyote ya presha lakini ngoja tuone ni vipi wanaenda kumudu hali
hiyo tunapoenda kwenye mapambano ya mwisho.”
0 comments:
Chapisha Maoni