Viongozi wa Korea Kaskazini walitembelea saluni moja
iliyoko mjini London, kutaka kujua ni kwa nini walitumia picha ya
kiongozi wao Kim Jong-un katika bango la kibiashara.
Bango hilo lenya picha ya rais huyo, lilitumiwa kutangaza kupunguzwa kwa bei ya kunyolewa katika saluni moja.
Bango hilo katika M&M Hair
Academy lilikuwa na picha ya kiongozi huyo wa Korea Kaskazini pamoja na
maneno "Bad Hair Day?" yaani je unahitaji kutengezwa nywele?....
Kinyozi kwa jina Karim Nabbach alisema kuwa
maaafisa wa ubalozi wa Korea walifukuzwa na mkurugenzi wa saluni hiyo
walipojaribu kuingia katika saluni hiyo huku wakiwa wakali wa maneno.
Polisi nao kwa upande wao wamesema kuwa walizungumza na pande zote mbili husika na hakuna kosa lolote lilibainika.
Picha iliyozua mgogoro |
Saluni hiyo ilibandika bango hilo tarehe 9
Aprili na keshoye wakapokea wageni wawili waliodai kuwa walikuwa
maafisaa wa ubalozi wa korea kaskazini walio taka kumwona mkurugenzi wa
saluni hiyo
Karim Nabbach amenukuliwa akisema kuwa waliweka
mabango ya kutangaza kupunguzwa kwa bei ya kunyolewa kwa wanaume katika
mwezi Aprili.
Bango hilo lilitokana na habari za hivi karibuni
kuwa wanaume wa Korea wametakiwa kunyoa nywele kwa mtindo mmoja tu kama
alivyonyolewa Rais Kim Jong Un.
Mkurugenzi wa saluni hiyo anasemekana kuwa
aliwaeleza wageni wake kuwa walikuwa nchini uingereza nchi ya
kidemokrasia na kuwataka waondoke kwenye saluni yake na kisha
aliwafahamisha polisi kuhusu yaliyotokea pamoja na ubalozi wa Korea
Kaskazini kuwa alikuwa amewasiliana na polisi.
Akizungumza na kipindi cha BBC radio 4 Karim
Nabbach alisema kuwa kutoka wakati ule hawakupata shida yeyote ile na
kuwa licha ya hayo bango hilo liliwavutia wateja wengi waliodhania kuwa
lilikuwa la kuchekesha.
Wakati huo huo aliongeza kuwa bango hilo
halikuwa linatumika kisiasa mbali lilitumika tu katika matangazo yao ya
kibiashara ili kuwavutia wateja.
Mwezi uliopita Radio Free Asia iliripoti kwamba
wanafunzi wa kiume katika vyuo vikuu vya korea kaskazini walitakiwa
kunyoa nywele yao kwa mtindo sawa na ule wa kiongozi wao.
0 comments:
Chapisha Maoni