Klabu ya Arsenal ilikuwa lazima
iifunge Wigan kwa penati lakini walishindwa kuonyesha nia kutokana na
jinsi walivyocheza licha ya kushinda katika mchezo huo wa nusu fainali
ya kombe la FA.
Mchambuzi mahiri wa soka,Paul Merson anakiri
kuwa Arsenal walikuwa na bahati sana kuifunga timu hiyo ya Championship
na anasema yalikuwa matokeo makubwa sana kwa kikosi hicho cha Arsene
Wenger kutinga fainali.
Lakini akasisitiza,”Kama wanataka kuingia
katika nne bora,wanahitaji kujifunza kutoka hapa kwasababu kama
wanacheza kwa jinsi walivyocheza Jumamosi mpaka mwisho wa msimu basi
hawawezi kupata nafasi ya kushiriki ligi ya mabingwa barani Ulaya.”
Huku akisema majeruhi hayajawasaidia kwani
wachezaji kama Aaron Ramsey na Theo Walcott hawawezi kuwa wachezaji wa
kiwango cha dunia lakini ni wachezaji muhimu na hodari zaidi kwa
Arsenal.
Na kuongeza kuwa bila Theo wamekuwa wakipata tabu sana wakati Wenger
amekuwa akiwatumia chipukizi,Yaya Sanogo mbele ya Olivier Giroud lakini
haijasaidia kitu katika timu.
Merson akasisitiza kuwa mfaransa huyo inabidi abadilishe hiyo staili
pindi atakapocheza na West Ham na kumchezesha kiungo mmoja mshambuliaji
kwasababu vijana wa Sam Allardyce wataenda Emirates Stadium kupaki basi.
Pia akasema alipoangalia ratiba alihisi mchezo
huo utakuwa mgumu sana hivyo akakiri kuwa Arsenal wanapaswa kucheza kwa
kujiamini,kujituma na kutafuta magoli ya mapema zaidi.
Mwisho akasema kuwa mchezo huo Arsenal wanaenda na kushinda 2-0.
0 comments:
Chapisha Maoni