ASKOFU Mkuu wa Kanisa la Full Gospel & Bible Fellowship (FGBF) lenye
makao makuu yake jijini Dar es Salaam, Zakaria Kakobe ameibuka na
kuweka wazi kuwa kuonekana kwa Mwezi Mwekundu (Blood Moon), Aprili 15,
mwaka huu ni ishara kuu ya mwisho wa dunia kama maandiko yanavyosema
katika Matendo 2:17-21.
Askofu Kakobe aliyasema hayo juzi kufuatia tukio hilo lililojiri siku
tano kabla ya Sikukuu ya Pasaka ambapo mwezi wote ulipatwa (lunar
eclipse) na kuwa mwekundu kama damu, tukio ambalo pia litatokea tena
mwakani.Kufuatia tukio hilo lenye kuogofya, baadhi ya mitandao ya
kijamii duniani kote imekumbushia maneno ya manabii mbalimbali lakini
zaidi kutoka kwenye Biblia wakisema mwisho wa dunia sasa ni dhahiri.
Kinachotakiwa kwa watu sasa ni kuacha maovu na kumrudia Mungu. Ni wajibu wa kila mtu kujiweka tayari kwa kuokoka kwani bila kufanya hivyo watakaokutwa katika dhambi watatupwa jehanamu
alitahadharisha Askofu
Kakobe.
Aliongeza kuwa, dalili zote za mwisho wa dunia zilizotajwa katika
Biblia ziko wazi kwa sasa, kama vile hilo la mwezi wa damu, kuzuka kwa
manabii wa uongo, vita ya nchi na nchi na ukoo kwa ukoo lakini akasema
hajui ni kwa nini watu hawataki kuokoka.
Naye Mchugaji wa Kanisa la Assemblies of God ‘Mikocheni B’ la jijini
Dar, Mama Getrude Rwakatare alikiri kulijua hilo la mwezi kuwa wa damu
na kusema katiba Biblia, Luka 21:25 Mungu amefafanua kuwa kuna dalili
mbalimbali zitajitokeza siku za mwisho wa dunia na sasa zinaanza
kuonekana, akawataka watu kuomba bila kuchoka.
Dalili nyingine ni mataifa kupigana, upendo wa wengi kupoa, manabii wa uongo kuibuka na kadhalika. Haya tunayaona sasa, hivyo watu wote tumrudie Mungu
alisema Mama Rwakatare.
Nabii Nicolaus Suguye wa Kanisa la
Huduma na Neno la Upatanisho ambaye alisema dalili za mwisho wa dunia ni
nyingi ambazo ni mataifa kupigana, kukosa uhusiano mzuri na kuzuka kwa
manabii wa uongo.
Uwazi lilikwenda mbele zaidi kwa kuzungumza na kiongozi wa Kanisa la
Ngurumo za Upako lenye makao makuu jijini Arusha, George David
‘GeoDavie’ ambapo alikuwa na haya ya kusema:
Suala la kupatwa kwa mwezi na kuwa damu ni ishara ya mwisho wa dunia lakini nasisitiza kuwa pia ni jambo la kisayansi zaidi.
Alizidi kusema kuwa kilichoandikwa kwenye Biblia, Luka 21:25 (Tena
kutakuwa na ishara katika jua na mwezi na nyota na katika nchi, dhiki ya
mataifa wakishangaa kwa uvumi wa bahari na msukosuko wake) lazima
kikubalike na kila anayemwamini Mungu.
Mchungaji Imani Mwakyoma wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God
(TAG) Magomeni jijini Dar, yeye alisema kupatwa kwa mwezi na kuonekana
wa rangi ya damu ni mafundisho ambayo watumishi wa Mungu wamekuwa
wakiihubiri kila kukicha.
Tumekuwa tukihubiri kwa muda wa miaka kumi sasa kwamba mwisho utafika pale tu ishara ya anga itakapoanza kuonekana, mwezi kuwa wa damu na jua kuwa giza, siku hizi kila mara jua linapatwa na kuwa giza, bado nini sasa hapo? Watu wamrejee Mungu
alisema Mchungaji Mwakyoma.
Baadhi ya waumini wa kanisa la Romani Katoliki linaloongozwa na Mwadhama
Polycarp Kardinali Pengo na Kanisa la KKT linaloongozwa na Askofu Dr.
Alex Gerhaz Malasusa, walisema watumishi hao wa Mungu mara kwa mara
wamekuwa wakihubiri watu kutubu kwa kuwa siku za mwisho wa dunia zipo
dhahiri kwa sasa.
Naye John Hagee, Mchungaji wa Kanisa la Cornerstone, San Antonio, Texas
Marekani na mwanzilishi wa muunganiko wa Wakristo nchini Israeli
alishawahi kutoa kitabu akiongozwa na taasisi ya uchunguzi wa anga za
juu ya nchi hiyo, NASA kwa kufanya makadirio kupitia historia ambapo
aliandika uhusiano wa moja kwa moja kati ya kupatwa kwa mwezi na kuwa
mwekundu na utabiri wa Waisrael na wanadamu wote.
Katika kitabu hicho, Mchungaji Hagee aliandika kwamba, zaidi ya miaka
500 iliyopita kupatwa kwa mwezi wa damu kulitokea siku ya kwanza ya
Sikukuu ya Pasaka mara tatu tofauti.'
Hata Aprili mwaka huu, mwezi huo ulipatwa na kuwa mwekundu kuelekea
Sikukuu ya Pasaka na itatokea tena mwakani kipindi cha Pasaka.
Mchungaji Hagee alifafanua kwamba kupatwa kwa mwezi ni lazima watu, hasa
Wakristo waelewe ishara hizo. Alisema katika Biblia, Joel: 2 na
Matendo ya Mitume: 2 vyote vimeandika tukio hilo kwamba ndiyo mapito ya
dunia kuelekea mwisho wake.
Kwa mujibu wa Markell, mchambuzi wa mambo ya sayansi, kupatwa kwa mwezi
na kuwa wa damu kutatokea tena katika mpangilio wa Oktoba 8, 2014,
Aprili 4, 2015 na Septemba 28, 2015!
Hata hivyo, Markell anasema kuwa Wakristo wengi wanaamini maneno ya
kale kwamba kupatwa kwa mwezi ni dalili ya ujio wa pili wa Kristo na
hivyo kusababisha hofu miongoni mwa wale ambao hawajui maana halisi japo
maelezo ya kisayansi yanafafanua jambo hili.
Alisema kimsingi, rangi ya mwezi ni nyekundu ambayo ipo katika anga
ya dunia na kama dunia haina anga, moja kwa moja mwezi utafunikwa na
giza.
Markell ambaye anaamini kwamba shetani yupo nyuma ya harakati za
maendeleo, anasema hakuna mtu anayejua ishara za mwezi lakini
alipendekeza kuwa dunia inapaswa kubashiri kwa habari mbaya.
0 comments:
Chapisha Maoni