Jumanne, Aprili 29, 2014

MUME NA MKE WATEKWA NA WATU WASIOJULIKANA

Dickson Mathias (35), na msichana aliyejulikana kwa jina la Mariam Kimaya wanadaiwa kutekwa kwa nyakati tofauti baada ya kufunga ndoa ya siri katika Kanisa la KKT, Tegeta jijini Dar, Mei Mosi, 2012.
Akielezea tukio hilo dada wa Dickson, Aneth Mbaga alisema tukio hilo lilitokea baada ya Dickson kufunga ndoa hiyo na Mariam bila idhini ya wazazi wake kwenye kanisa hilo.
Mariam Kimaya
Baada ya habari za kufunga ndoa ya siri kanisani kuwafikia baadhi ya ndugu wa Mariam, Dickson alianza kupokea simu za vitisho wakimuuliza ni kwa nini alifunga ndoa ya siri na binti yao wao wakiwa hawajui?
Agosti 10, mwaka jana, nikapata taarifa kwamba Dickson alitekwa maeneo ya Mbezi ya Jogoo (Dar) na watu wasiojulikana.

alisema Aneth.
Aneth alizidi kuongeza kuwa miezi minne mbele, alipata taarifa kuwa,  mkewe Mariam naye alitekwa na watu wasiofahamika, hadi sasa hajulikani alipo kama vile mumewe.
Dickson Mathias
Yeyote mwenye taarifa sahihi naomba aripoti kituo chochote cha polisi kilicho jirani yake maana ndugu tuna wasiwasi mkubwa, hata kwa ndugu wa mwanamke nako hakuna anayejua waliko wawili hao
alisema dada huyo huku akimwaga machozi.
Taarifa za kutekwa kwa Dickson ziliripotiwa katika Kituo cha Polisi Tabata na kuandikiwa jalada: TBT/RB/1988/2013 na polisi bado wanawasaka wanandoa hao.

0 comments:

Chapisha Maoni