Jumatano, Aprili 30, 2014

COSTA: CHELSEA HAWATAPAKI BASI, WATASHAMBULIA


Mshambuliaji wa Atletico Madrid, Diego Costa anaamini kuwa Chelsea hawatatumia mbinu yao ya kujilinda katika mchezo wa nusu fainali ya pili ya UEFA leo dimbani Stamford Bridge.

Jose Mourinho alitumia mbinu ya `Kupaki basi` katika mechi ya kwanza uwanja wa Vicente Calderon na kulazimisha suluhu ya bila kufungana na alitumia mbinu kama hiyo kuwafunga Liverpool mabao 2-0 jumapili iliyopita katika mchezo wa ligi.
Hata hivyo, Costa akiyezaliwa Brazil lakini ana uraia wa Hispania anatarajia kuona Chelsea ikishambulia zaidi katika mechi ya kesho jumatano kwa malengo ya kufika fainali.
Sina shaka, ni mchezo mkubwa, acha tufurahi na kuucheza; itakuwa mechi tofauti kwa wenyeji, watajitahidi kucheza kwa kushambulia zaidi
 alisema Costa.

RATIBA | UEFA 2013-14
Champions League
Leo Jumatano
21:45 Chelsea vs Atlético Madrid

Europa League
Alhamisi
22:05 Juventus vs Benfica
22:05 Valencia vs Sevilla

Ukuta wa Chelsea na Mashambulizi Ya Atletico Madrid, unaipa timu gani nafasi ya kuingia fainali?

0 comments:

Chapisha Maoni