
Mtoto Ali Yakubov mwenye umri wa miezi tisa amepata umaarufu mkubwa na amekuwa gumzo dunia nzima baada ya taarifa za miujiza yake ambapo maneno tofauti tofauti ya kiarabu kuanza kutokea kwenye mwili wake.
Maandishi
ya kiarabu yanayonukuu aya za Quran yamekuwa yakitokea kwenye mikono
yake, miguu na tumboni na kisha kutoweka baada ya siku kadhaa na kisha
maandishi mengine ya kiarabu yanayonukuu vipande tofauti vya aya za
Quran hujitokeza upya.
Madaktari nchini Urusi hadi leo bado
hawajui nini kinaendelea kwenye mwili wa mtoto huyo ambaye maandishi ya
kwanza ya kiarabu yanayosema neno "Allah" yalijitokeza kwenye kidevu
chake ndani ya wiki moja baada ya kuzaliwa.
0 comments:
Chapisha Maoni