Jeshi la polisi Mkoani Iringa linamshikilia dereva wa gari no:STK 5636 Aina ya Toyota Land Cruiser kwa tuhuma za kusababisha kifo cha mtu mmoja kwa ajari ya barabarani.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa jeshi la polisi Mkoani Iringa ACP Ramadhani Mungi amesema David Kumwenda mwenye umri wa miaka 47 mkazi wa eneo la Kihesa Manispaa ya Iringa anashikiliwa kwa tuhuma ya kusababisha kifo cha Mika Mhemela mwenye umri wa miaka 16.
Ameongeza kuwa ajali hiyo imetokea maeneo ya Kising’a Isimani barabara kuu ya Iringa –Dodoma wilaya ya Iringa Vijijini Mkoa wa Iringa na marehemu amefariki wakati anaendelea na matibabu.
Hata hivyo Kamanda Mungi amesema gari hilo ni mali ya Manispaa ya Iringa pia ametoa wito kwa madereva na wamiliki wa magari kuwa makini wawapo barabarani kwa kuzingatia sheria za usalama barabarani ili kupunguza ajari zianazoweza kuepukika.

0 comments:
Chapisha Maoni