Jumatano, Aprili 30, 2014

MAMBO MAKUBWA YALIYOTOKEA SIKU KAMA YA LEO DUNIANI KOTE

Leo ni Jumatano tarehe 30 Aprili 30, 2014, Siku kama ya leo miaka 237 iliyopita inayosadifiana na tarehe 30 Aprili 1777 Miladia, alizaliwa Carl Friedrich Gauss mwanahesabati na mnajimu wa Kijerumani. Mama wa Gauss ndiye aliyemshawishi mno mwanawe ajikite zaidi katika somo la hesabati, na hatimaye mtoto huyo alitabahari kwenye fani hiyo. Msomi huyo wa hesabati na mnajimu mashuhuri wa Kijerumani alifariki dunia akiwa na umri wa miaka 78.

Tarehe 30 Aprili mwaka 1945 dikteta wa zamani wa Ujerumani Adolf Hitler alijiua akiwa mafichoni chini ya ardhi baada na kufeli ndoto yake ya kutawala dunia nzima. Hitler alizaliwa mwaka 1889 nchini Austria na alipigana Vita vya Kwanza vya Dunia katika safu za kwanza za askari wa Ujerumani. Adolf Hitler alianzisha chama cha National Socialist German Workers baada ya kuchanganya itikadi za kisoshalisti na mitazamo mikali ya utaifa. Na ulipotimia mwaka 1939 alianzisha Vita vya Pili vya Dunia.

Na siku kama ya leo miaka 44 iliyopita alifariki dunia malenga, mwandishi na msanii wa uchoraji wa zama hizi wa Iran, Ustadh Ismail Ashtiyani. Baada ya masomo ya msingi na upili, Ustadh Ashtiyani alijifunza sanaa ya kuchora kwa msanii mashuhuri wa zama hizo Kamalul Mulk. Mwaka 1307 Hijria Shamsia alishika wadhifa wa mkuu wa Chuo cha Sanaa cha Darul Funun. Miongoni mwa vitabu vyake ni pamoja na diwani ya mashairi, Kumbukumbu ya Ulaya na Historia ya Kamalul Mulk.

Na siku kama ya leo miaka 125 iliyopita tarehe Mosi Mei ilitangazwa rasmi kuwa 'Siku ya Wafanyakazi Duniani'. Tarehe Mosi Mei 1886, zaidi ya wafanyakazi elfu 40 walifanya maandamano katika mji wa Chicago nchini Marekani kwa shabaha ya kudai haki zao. Wafanyakazi hao walitaka nyongeza za mishahara, kuboreshwa suhula za maeneo yao ya kazi na uadilifu kazini. Maandamano hayo yaliingiliwa na askari polisi na matokeo yake idadi kubwa ya wafanyakazi hao waliuawa na wengine kujeruhiwa.

0 comments:

Chapisha Maoni