Jumanne, Aprili 29, 2014

KUTOKA FACEBOOK LEO NIMEKUTANA NA TOFAUTI ZA NDOA ZA ZAMANI NA SASA

1. Zamani wanaume walioa na wanawake waliolewa. Kila mmoja alitimiza majukumu yake vyema na kwa staha kubwa. Siku hizi watu wanaoana. Majukumu yote ni ya wana ndoa bila kujali jinsia.
2. Zamani wanawake walikuwa wasikivu kwa waume zao, utii ulikuwa juu. Siku hizi wanawake wabishi kinoma. Wanatafuta tuzo za ubishi kwenye familia.
3. Zamani wanawake walivaa kanga, sketi, gauni n.k siku hizi ni mwendo wa suruali za kubana na nguo za ajabu ajabu boobs nje nje.

4. Zamani tendo la ndoa mpaka mkioana, siku hizi bibi harusi anaolewa ana mimba au mtoto wao wa kwanza nansimamia harusi
5. Zamani ndoa zinadumu hadi kifo...siku hizi unaoa leo jumamosi ikifika Jumatano mshaachana
6. Zamani mume alimzidi Mke miaka 6+ vipi hili bado linazingatiwa kweli?
7. Zamani wanaume walikuwa wakihudumia familia zao bila mchango wa wake zao. Lakini sasa wanatafuta wanawake wenye kazi ili wapige pasu katika kutoa matumizi ya familia.

0 comments:

Chapisha Maoni