Wanafunzi wanao tarajia kufanya mitihani ya kuhitimu elimu ya kidato cha sita nchini wametakiwa kutumia muda uliobaki kwa ajiri ya maandalizi ya mtihani wa kumaliza masomo yao.
Akizungumza kwa niaba ya mkuu wa Mkoa wa Iringa,Bw Gerald Guninita ambae pia ni mkuu wa wilaya ya Kilolo aliekuwa mgeni rasmi,wakati alipokuwa akipokea risala iliyosomwa na wanafunzi wanao maliza masomo yao katika shule ya Sekondari Mwembetogwa iliyopo Manispaa ya Iringa ambapo amesema ni vyema wakatumia muda huu mchache ulibaki kwa ajiri ya kuendelea kujiandaa zaidi katika kukabilia na mtihani wao utakaoanza May 5 mwaka huu.

Mkuu wa wilaya huyo amesema kuwa mara baada ya kumaliza masomo yao,watakwenda kwao hivyo elimu waliyoipata wakaitumie vizuri kwa kuwa mabalozi wazuri katika suala la nidhamu na kukataa kutumiwa na wanasiasa hususani katika suala hili linalo endelea sasa la mchakato wa kupata katiba mpya.
Aidha Guninita ameongeza kuwa wapo wanasiasa watako fanya mikutano na maandano kwa kuwashirikisha vijana na kuwapatia pesa ili kuleta vurugu kitendo ambacho kinaweza kuhatarisha amani na maisha yao,hivyo wahakikishe kuwa hawajihusishi kwa namna yeyote katika vitendo hivyo.
Pia amewataka wazazi kushiriki kikamilifu katika kutoa michango mbalimbali ya maendeleo katika elimu,na kuacha kuchangia michango mingine isiyo na tija katika jamii.
Hata hivyo kwa upande wake Mkuu wa Shule hiyo mwalimu Kelvin Mlengule amesema kwa sasa wapo kwenye mchakato wa kuhakikisha wanapata vitanda kwa ajiri ya mabweni ya wasichana ambayo tayari yamekwishamilika,huku wakiendelea na mpango wa kujenga mabweni mengine ya wavulana,ambapo kwenye maafari hayo wamepata mchango wa zaidi ya shilingi milioni 10 zikiwemo ahadi kutoka kwa wadau mbalimbali walio hudhuria mahafari hayo.

0 comments:
Chapisha Maoni