NAHODHA wa Burundi, Didier Kavumbangu amesaini Mkataba wa miaka
miwili na mabingwa wapya wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Azam FC
mchana wa leo.
Kavumbangu aliyemaliza Mkataba wake wa miaka miwili Yanga SC, ameamua
kusaini Azam FC baada ya kuona klabu yake haina mawasiliano naye licha
ya kumaliza Mkataba wake.
Mimi ni mchezaji, kazi yangu ni mpira. Nimemaliza mkataba Yanga, lakini viongozi hawaniambii kitu, nimepata ofa nzuri Azam nikaamua kusaini
amesema Kavumbangu baada ya kusaini
Mkataba huo ambao unamfanya alipwe vizuri kuliko alivyokuwa analipwa
Jangwani.
Pamoja na hayo, Kavumbangu ameishukuru Yanga SC na mashabiki kwa
miaka miwili aliyoichezea timu hiyo na anasema itabakia kwenye
kumbukumbu zake kwa ameshinda nayo mataji.
Mshambuliaji huyo mrefu mwenye nguvu amesema sasa akili yake
anaipeleka kwa mwajiri wake mpya, Azam FC ambako pia amepania kwenda
kushinda mataji na kuiwezesha timu hiyo ya Alhaj Sheikh Said Salim Awadh
Bakhresa na familia yake kufanya vizuri kwenye michuano ya Afrika.
Mimi sasa ni mchezaji wa Azam, nafurahi kujiunga na klabu hii kubwa. Kawaida yangu huwa nashabikia klabu nayochezea, sasa mimi ni mshabiki namba moja wa Azam
amesema.
Tukutane Chamazi; Kavumbangu anahamisha virago vyake kutoka Jangwnai hadi Chamazi
Kavumbangu alitua Yanga mwaka 2013 akitokea Atletico ya Burundi na katika mechi misimu miwili ya kuichezea klabu hiyo, amefunga mabao 31 katika mechi 63 za mashindano yote, moja tu la penalti.

0 comments:
Chapisha Maoni