Watu 13 kiwemo askari wa kikosi cha usalama barabarani wamepoteza
maisha baada ya kugongwa na basi la kampuni ya Sumry lililokuwa likitoka
Kigoma kwenda Dar katika kijiji cha Ikungi mkoani Singida usikuwa kuamkia leo.
Ajali hiyo ilitokea baada ya ajali ya kwanza iliyolihusisha lori
lililomgonga mwendesha baiskeli aliyepoteza maisha papo hapo na wakati
wananchi wakiwa wamekusanyika eneo hilo la ajali huku trafiki akiendelea
kupima ajali hiyo, lilitokea basi la kampuni ya Sumry na kuwagonga watu
hao pamoja na trafiki na kupelekea jumla ya watu 14 kupoteza maisha
eneo hilo.
Basi hilo lililokuwa likitokea Kigoma kwenda Dar halikuweza kusimama eneo hilo mpaka dereva wake alipokwenda kujisalimisha kituo cha polisi Ikungi, Singida. Miili 14 ya waliopoteza maisha katika ajali hiyo imehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa mkoani Singida pamoja na majeruhi wawili waliopelekwa hospitalini hapo.

0 comments:
Chapisha Maoni