Binti mmoja aliyetambulishwa kwa jina la Fauzia (jina la mbele lipo),
mwenye umri wa miaka 16, mkazi wa Kigogo jijini Dar amedai kutumikia
nafasi ya umalkia katika imani yenye utata duniani ya Freemason.
Binti huyo alikwenda mbele zaidi kwa kudai kwamba ili kujiunga na imani hiyo, alimuua mama yake mdogo kwa ajili ya kafara.
Akizungumza siku chache baada ya kuokoka akiwa
nyumbani kwa baba yake mdogo, Kigogo, Fauzia alisema alitokea Wilaya ya
Kahama mkoani Shinyanga alipokuwa akiishi na bibi yake.
Alikuja Dar kwa lengo la kuendeleza mauaji ya kafara ambapo safari
hii ilikuwa amuue mama yake mdogo mwingine ambaye ni mjamzito kwa sasa.
Alisema kama angefanikiwa kumuua, angepandishwa cheo na kuwa malkia kamili katika jamii hiyo inayotafsiriwa vibaya duniani.
ALIKOTOKEA
Fauzia alisema kuwa mara ya kwanza hakujua kama amekuwa mwanachama wa Freemason bali alichojua yeye alijiunga na uchawi wenye ushirika wa Kahama na Kigogo jijini Dar es Salaam ambapo mara kwa mara alikuwa akija Dar usiku na kufanya mambo ya kichawi kwa watu mbalimbali.
Fauzia alisema kuwa mara ya kwanza hakujua kama amekuwa mwanachama wa Freemason bali alichojua yeye alijiunga na uchawi wenye ushirika wa Kahama na Kigogo jijini Dar es Salaam ambapo mara kwa mara alikuwa akija Dar usiku na kufanya mambo ya kichawi kwa watu mbalimbali.
Alisema siku moja aliambiwa lazima amtoe uhai mama yake mdogo, naye
kwa uwezo aliokuwa nao alifanya hivyo, mama yake mdogo akafa kwa kuugua
ghafla.
Baada ya kifo cha mama yake mdogo, ndipo usiku mmoja bibi kizee mmoja
(alimtaja jina) alimtokea katika ulimwengu wa kiroho na kumwambia
alitakiwa aende kwenye Jiji la Lagos nchini Nigeria kwa ajili ya
kutambulishwa rasmi na kupewa umalkia mdogo.
SAFARI YA NIGERIA ILIVYOKUWA
Akiendelea kuzungumza huku akionekana kujiamini licha ya umri wake mdogo, Fauzia alisema:
Akiendelea kuzungumza huku akionekana kujiamini licha ya umri wake mdogo, Fauzia alisema:
Siku nilipoondoka kwenda Nigeria nilikuwa na wenzangu walionisindikiza. Ilikuwa ni safari ya kimiujiza. Tulipofika kule, wao waliniacha mahali, mimi nikajikuta nikitokea ndani ya jengo kubwa ambalo ndani yake nilikuta mtu mwenye asili ya Kiarabu.
Yule mtu alinipokea na kuishi naye. Siku moja aliniambia Fauzia wewe una na nguvu mbili, za Freemason na uchawi
alisema.
ASIMIKWA KUWA MALKIA MDOGO
Aliendelea kusema:
Aliendelea kusema:
Ndipo siku moja ikafika, nikasimikwa kuwa malkia mdogo kwa kukabidhiwa gauni fupi jeupe na kitambaa cheupe cha kuvaa kichwani (vilioneshwa kwa waandishi wa habari hii).
Hizi nguo ni dalili kwamba anayemiliki ni malkia mdogo. Unakuwa na uwezo wa kujua mambo yote ya siri ya kidunia yanayoendelea.
Baada ya hapo, nilirejea hapa nchini kwetu. Nilipokewa na bibi ambaye alikuja kimazingara. Bibi aliniuliza ni wapi nilikokuwa mpaka nimepata nguvu za Freemason wakati yeye alinikabidhi uchawi wa kawaida? Sikumjibu
alisema Fauzia mbele ya baba yake mdogo na mama yake mdogo
aliyekuwa amuue.
AKUMBUKA SIKU YA KWANZA KUJIUNGA NA FREEMASON
Katika mazungumzo hayo yaliyohudhuriwa pia na majirani, binti huyo akakumbuka jambo zito lililomtokea akiwa darasa la saba na kusema:
Katika mazungumzo hayo yaliyohudhuriwa pia na majirani, binti huyo akakumbuka jambo zito lililomtokea akiwa darasa la saba na kusema:
“Nakumbuka nikiwa darasa la saba, siku moja usiku niliota ndoto.
Nilimwona mzee mmoja mwenye mapembe akinijia na kunikabidhi mikoba.
Naamini yule mtu ndiyo aliniingiza kwenye Freemason kwani kuanzia pale
ndipo nilipobadilika na kuwa na uwezo wa kuja Dar na kurudi Kahama kwa
usiku moja.
“Basi, baada ya kurudi nyumbani Kahama, siku moja nikaambiwa na
wakubwa wangu natakiwa kwenda nchini Marekani kwa ajili ya kuongeza
nguvu za Freemason.
“Kule nilikaa kwa siku kadhaa na nikafundishwa mambo mengi ya ajabu,
pia nilikutana na viongozi wakubwa wa kidini na kiserikali wa hapa
nchini Tanzania (aliwataja majina).
MAISHA YA NYUMBANI AKIWA SAFARINI
Ilivyokuwa ni kwamba, kila nilipokuwa safarini, nyumbani nilikuwa naacha jini lililofanana na mimi kwa kila kitu. Jini hilo lilifanya kazi nyumbani badala yangu pasipo mtu yeyote kufahamu wakijua ni mimi. Niliporudi na jini liliondoka.
ATOBOA SIRI ZA SCREEN TOUCH
Nikiwa katika jengo la ajabu la Freemason nchini Marekani, niliona watu wengi wakitengeneza simu za kisasa ‘screen touch’ na televisheni za ‘flat screen’ nilipowauliza za nini? Walinijibu kuwa simu hizo zimewekwa kifaa maalumu cha kunyonya damu ya mtumiaji kutoka kwenye kidole chake kila mara atakapobofya.
Zamani kulikuwa na simu zikitumia peni maalum kwenye screen lakini Freemason waliamua kuziondoa kwa kuwa hazikuwa zikiwapelekea damu. Hivyo mtumiaji wa simu za screen touch za sasa lazima aguse kwa kidole chake na si kwa kitu kingine ndipo ataweza kutumia simu yake ilimradi tu achangie damu yake kwenye benki za damu za Freemason zilizopo Marekani.
KUHUSU TV FLAT SCREEN
Akifafanua kuhusu runinga za flat screen, Fauzia alisema kuwa, hizo zimewekewa kifaa chenye mionzi ya ki-Freemason ambacho humfanya mtu anayeangalia kila wakati kuwa zezeta huku vifo vya ghafla akivitaja kama matokeo makuu ya kuangalia televisheni hizo.
0 comments:
Chapisha Maoni