Jumanne, Machi 11, 2014

HUYU NDIO MODEL MAARUFU TOKA UINGEREZA UTAKAYEMUONA KATIKA VIDEO MPYA YA OMMY DIMPOZ, ANAITWA SOFIA SKVORTSOVA


Hivi karibuni Ommy Dimpoz alishoot video ya wimbo wake mpya jijini London Uingereza na muongozaji maarufu barani Afrika na Ulaya, Moe Musa ambaye ameshoot video za mastaa kibao zikiwemo Antenna na Azonto za Fuse ODG, Caro ya Wizkid na Skelewu ya Davido.
Model atakayeonekana kwenye video hiyo ni maarufu sana jijini London aitwaye Sofia Skvortsova. Sofia Skvortsova alizaliwa na kukulia Riga, Latvia. Ana asili ya Urusi, Ujerumani na Poland.

Kazi yake ya umodel hufanyia jijini London hufanya kazi na mawakala wa mamodel. Amekuwa akifanya shughuli hiyo kwa zaidi ya miaka mitano barani Ulaya na Mashariki ya Kati.
Ameshaonekana kwenye majarida kibao, filamu, matangazo na video za muziki.

0 comments:

Chapisha Maoni