Ngaweje Said (39), mkazi wa Kijiji cha Zinga, Bagamoyo, Pwani anateseka
na gonjwa asilolijua ambapo nyama kubwa imeota toka juu ya uso upande wa
kushoto na kumwagikia kifuani, Uwazi lilikutana naye uso kwa uso.
Akizungumza na mwandishi wetu akiwa nyumbani kwake kijijini hapo juzi, Ngaweje alisema:
“Ugonjwa huu ulinianza nilipozaliwa tu mwaka 1975 pale Hospitali ya Bagamoyo. Kilianza kipele, lakini kadiri nilivyokuwa nikikua, kipele nacho kilikua.
“Ugonjwa huu ulinianza nilipozaliwa tu mwaka 1975 pale Hospitali ya Bagamoyo. Kilianza kipele, lakini kadiri nilivyokuwa nikikua, kipele nacho kilikua.
“Sikujua kama itafikia hali hii. Hata wazazi wangu nao hawakujua, waliamini baada ya tiba kipele kitanywea, lakini wapi!
“Baadhi ya watu walishauri nipelekwe Hospitali ya Muhimbili ambako
kuna madaktari bingwa. Kweli, mwaka 1979, baba alinipeleka Muhimbili
ambako nilipata tiba na kurudi nyumbani lakini kipele kilizidi kukua.
“Mwaka 1995, mimi mwenyewe nilirudi tena Muhimbili. Safari hii madaktari waliniambia watanifanyia upasuaji kwa awamu.
“Mwaka 1995, mimi mwenyewe nilirudi tena Muhimbili. Safari hii madaktari waliniambia watanifanyia upasuaji kwa awamu.
“Walinifanyia upasuaji, wakaniruhusu kurudi nyumbani ili nikatafute
fedha halafu nirudi tena lakini hawakuniambia ni shilingi ngapi na pia
sikupata hiyo pesa!
“Mwaka 2001 sasa ikiwa si kipele tena bali ni linyama likubwa,
niliamua kwenda Hospitali ya CCBRT, (Msasani, Dar). Pale pia wakaniambia
nikatafute pesa halafu nirudi wanifanyie upasuaji.
“Sikuwa na fedha kwa sababu sikuwa na kazi yoyote ya maana, ni kama
nilivyo sasa. Kuanzia hapo niliamua kuachana na hospitali nikimtegemea
Mungu atakavyoamua.
“Mbaya zaidi wazazi wangu walishafariki dunia. Alianza baba, akaja mama kwa hiyo nikawa sina msaada wowote ule.
“Nilipanga kuoa nikiamini kwamba mke atanisaidia, lakini wanawake
wananikataa kwa hali yangu. Na ukiangalia ni kweli, mke gani atakuwa
tayari kuishi na mume mwenye linyama kama hili, tena usoni?
“Kwa sasa nahangaika tu, nafanya biashara ya kuchajisha simu za watu kwa shilingi 200 kwenye chumba nilichopewa. Kwa siku wanaweza kuja wateja wanne ambapo napata shilingi 800 tu, hainisadii chochote.

“Kusema ukweli jamani mimi nakufa, lakini kama Watanzania wenzangu
mpo na mtaguswa na gonjwa langu hili naombeni mniokoe. Kuna watu
wanasema nikienda India wanaweza kunifanyia upasuaji nikawa kama
binadamu wengine, lakini nitaendaje huko wakati sina fedha?”
Simulizi ya Ngaweje inaumiza sana, hata mazingira anayoishi si ya
kuridhisha. Anasema anahisi kichwani ana mzigo mzito kutokana na nyama
hiyo kumwelemea.
Anasema: “Hata nikitembea nahisi kuzidiwa upande mmoja. Nafsi yangu imekuwa ikijitenga na watu kwa sababu naamini siko kamili na pia nahisi nawakera wanaponiona.”
Anasema: “Hata nikitembea nahisi kuzidiwa upande mmoja. Nafsi yangu imekuwa ikijitenga na watu kwa sababu naamini siko kamili na pia nahisi nawakera wanaponiona.”

0 comments:
Chapisha Maoni