WATU wanaodaiwa kuwa ni wa imani ya Freemason wametua ndani ya ibada
katika Kanisa la Ufufuo na Uzima linaloongozwa na Mchungaji Kiongozi
Josephat Gwajima.
Kwa mujibu wa chanzo chetu, Freemason hao wawili waliingia kwenye ibada
hiyo iliyofanyika Februari 23, mwaka huu ndani ya kanisa hilo lenye
makao makuu yake katika Viwanja vya Tanganyika Peckers, Kawe jijini Dar
wakiwa na mfuko wa rambo wenye vitu mbalimbali vikiwa na alama zao.
Habari zilidai kwamba wakati neno likiendelea kunenwa na Mchungaji
Gwajima, watu hao walifunua mfuko huo ambapo baadhi ya waumini waliokuwa
karibu yao walihoji kulikoni kuwa kwenye ibada na vitu vyenye viashiria
ya Freemason.
“Wengine tulishangaa sana kwani baadhi ya vitu vilionekana kuwa na
thamani kubwa, tukadhani labda wameleta zawadi kwa mtumishi wa Mungu
(Gwajima),” kilisema chanzo hicho ambacho kinaabudu katika kanisa hilo.
Mtiririko wa tukio hilo unazidi kuwekwa wazi kwamba, haraka sana walinzi
wa kanisa hilo walifika eneo lenye mfuko huo na kuunasa huku watu
walioingia nao wakipotea au kujichanganya miongoni mwa waumini wengine.
Kufuatia tukio hilo, baadhi ya waumini wa kanisa hilo walipozungumza na
Uwazi baada ya ibada kumalizika walisema wanaamini watu hao walifika
kanisani hapo kwa nia mbili, kujisalimisha au kuzijaribu nguvu za
Gwajima ambaye ni maarufu kwa kuibua misukule.
Mashuhuda wa tukio hilo walisema kuwa, ndani ya mfuko wa watu hao
kulikutwa saa ya rangi ya fedha, pete ya dhahabu, cheni 2 za fedha,
bangili, fulana nyeupe na shati jeusi, vyote vikiwa na picha zenye alama
mbalimbali za Freemason kama mafuvu, nyoka na bikari.
“Lakini mimi naamini wale watu nia yao hasa ilikuwa kumjaribu
mtumishi wa Mungu ambaye ni kinara wa kuwarudisha watu waliokufa katika
mazingira ya mazingara (misukule),” kilisema chanzo kimoja na
kujitambulisha kwa jina moja la Isaya.
“Mimi ninavyomjua Gwajima sidhani kama wangefanikiwa, ni vigumu sana.
Kuna majambazi waliwahi kujaribu kumuua lakini waliambulia patupu,
wakapigwa na upepo wa kisurisuri, sembuse Freemason? Ninachokijua mimi
watamjaribu lakini hawataweza,” kilisema chanzo kingine.
Wakati sakata hilo likiendelea, mmoja wa waandishi wa Uwazi alipata
taarifa ambapo aliwahi tukio hilo na kujaribu kupiga picha lakini mlinzi
mmoja (jina tunalo) alimkataza licha ya kufanya jitihada kubwa.
Mlinzi huyo alimnyang’anya kamera mwandishi wetu na kuishikilia kwa muda huku akitishia kufuta picha zote hata kama hazikuwa za tukio hilo.
Mlinzi huyo alimnyang’anya kamera mwandishi wetu na kuishikilia kwa muda huku akitishia kufuta picha zote hata kama hazikuwa za tukio hilo.
Baada ya kuinyaka ishu hiyo nzima, Uwazi lilitumia siku tano kumsaka
Mchungaji Gwajima ili kupata mtazamo wake juu ya tukio hilo ambalo
huenda ni la kwanza kwenye kanisa hilo la kiroho jijini Dar es Salaam
lakini bila mafanikio kutokana na kukwamishwa na wasaidizi wake.
Awali, ilikuwa Februari 25, mwaka huu ambapo hakupatikana kanisani kwake na hata kwa njia ya simu.
Baada ya kumkosa mtumishi huyo kwa kutopokea simu, Uwazi lilimtumia ujumb
Baada ya kumkosa mtumishi huyo kwa kutopokea simu, Uwazi lilimtumia ujumb
e wa simu (SMS) na kumuuliza kuhusu tukio hilo na ikiwezekana kukutana ambapo alijibu kwamba alikuwa kwenye kikao cha viongozi wa Kikristo, Kurasini jijini Dar, hivyo asingeweza kuonana na wanahabari.
Ijumaa ya Februari 28, mwaka huu, waandishi wa gazeti hili walitumia saa tano kumsubiri Gwajima kanisani kwake bila mafanikio.
Baadaye msemaji wa kanisa hilo, Mchungaji Yeconia Bihagaze
alipoulizwa juu ya sakata hilo aliliambia gazeti hili kuwa, matukio kama
hayo hutokea mara kwa mara licha ya kuchukua muda mrefu ikilinganishwa
na hili la juzikati.
“Mambo ya Freemason kujisalimisha hapa mbona ni ya muda sana! Mimi
naona kama yamepitwa na wakati, tukio hilo unalolisema mimi sijalisikia.
Kanisa letu ni kubwa, mambo mengine ni madogomadogo hivyo siyo lazima
yafike kwenye uongozi wa juu.
“Kwa nini msiandike misukule tunaowafufua hapa kila siku? Kwa nini
msichukue matukio makubwa kwenye mtandao wa kanisa letu? Ninyi
wanahabari wakati mwingine huwa mnatuvunjia heshima ndiyo maana huwa
tunaamua kuwapotezea,” alisema Mchungaji Bihagaze.




0 comments:
Chapisha Maoni