Rooney: "Very happy to announce that I have signed a new extended contract with Manchester United" hiyo ni kauli ya Rooney.
STRAIKA wa Manchester United Wayne Rooney amefikia makubaliano ya Mkataba mpya utakaomweka Old Trafford hadi Juni 2019 na kumlipa Mshahara wa Pauni 300,000 kwa Wiki na kuweka Rekodi Klabuni hapo.
Mkataba wa sasa wa Rooney, mwenye Miaka 28, ulikuwa umalizike mwishoni mwa Msimu ujao na ulikuwa ukimlipa Pauni 250,000 kwa Wiki.
Rooney alijiunga na Man United Mwezi Agosti 2004 kutoka Everton na amebakiza Bao 42 tu kuifikia Rekodi ya Klabu ya kufunga Bao nyingi inayoshikiliwa na Sir Bobby Charlton alieifungia Man United Bao 249 enzi zake za Uchezaji.
Hadi sasa, Man United haijatangaza rasmi kusainiwa Dili hii.
Msimu uliopita kulikuwa na hatihati kwa Rooney kutaka kuihama Man United baada Meneja aliestaafu, Sir Alex Ferguson, kudai Rooney ameomba kuhama, kitu ambacho kilikanushwa na Mchezaji huyo.
Mwanzoni mwa Msimu huu, Chelsea mara mbili walitoa Ofa ya kumnunua Rooney na zote kukataliwa na Man United huku Meneja David Moyes akisisitiza Rooney atabakia Old Trafford na hauzwi kwa Bei yeyote.
Mwishoni mwa Januari, Rooney alirejea Uwanjani baada kuwa nje kwa Mwezi mmoja baada kuumia na hadi sasa, kwa Msimu huu, Rooney amecheza Mechi 28 kwa Klabu yake na kufunga Bao 11.

0 comments:
Chapisha Maoni