Wawili hao walipatana hivi karibuni wakiwa jijini Arusha.Akizungumza na gazeti namba moja la burudani Bongo, Ijumaa Wikienda, Jokate alisema ilipokaribia siku ya kwenda Arusha, Wema alimkaribisha kwenye shoo yake iliyofanyika jijini humo lakini alimwambia kuwa amebanwa ila akamuahidi kwamba akimaliza mambo yake atakwenda kumsapoti.
“Wema aliondoka bila kujua kama nitakwenda lakini nilipopanga ratiba
yangu ikakaa sawa, niliamua kwenda na kumfanyia ‘sapraizi’ na si kweli
kwamba nilisukumwa na nguvu ya pombe,” alisema Jokate.
Jokate alisema kwamba hakushauriwa wala kujadiliana na mtu yeyote
isipokuwa aliamua mwenyewe kufanya jambo hilo ambalo lilikuwa
likimkosesha faraja kwa muda mrefu.
“Nimeamua kumaliza mabifu kwa sababu nilikosa amani ninayoitaka kwa
muda mrefu. Ukweli Wema alinikaribisha, nikaona ndiyo sehemu ya kutimiza
lengo langu la kupatana naye,” alisema Jokate ambaye aliingia kwenye
gogoro na Wema baada ya kutembea na mpenzi wake, Nasibu Abdul ‘Diamond
Platnumz’.



0 comments:
Chapisha Maoni