
Taarifa za awali zilimtuhumu mmiliki wa nyumba ya wageni moja ambaye
pia anajihusisha na biashara za madini (jina tunalo) kwamba alimtoa
kafara mhudumu huyo. Ilidaiwa kuwa, kila mwaka mtu mmoja katika biashara
zake hupoteza maisha ghafla.
Hata hivyo, mfanyabiashara huyo alipoongea na Uwazi juzikati
alikanusha vikali tuhuma hizo na kueleza kuwa yeye ni muumini mzuri wa
imani yake.
‘’Hao watu wanapotosha sana, unajua kuna mwaka mwanaume mmoja alikufa
ghafla kwenye nyumba yangu ya kulala wageni, alikuja na mpenzi wake ila
alimeza Viagra ambazo hata polisi walizikuta mezani.
“Sasa watu wasio na nia njema na mimi tukio hilo wanaliunganisha na hili kwamba nawatoa kafara,” alisema.
“Sasa watu wasio na nia njema na mimi tukio hilo wanaliunganisha na hili kwamba nawatoa kafara,” alisema.
Kifo cha Blandina kilitokea ndani ya chumba huku mtu mmoja anayedaiwa
kuwa mpenzi wake aliyejulikana kwa jina moja la Timo, mkazi wa eneo
hilo akihojiwa na polisi.
Marehemu Blandina ambaye ni mzaliwa wa mkoa wa Tanga, anaelezwa na
bosi wake huyo kwamba alikuwa kama mtoto wa familia yake kwa vile
alimwamini sana. Alifanya kazi hapo kwa miaka 8 na hakuwa na tatilo la
kiafya.
Bosi huyo alisema mwili wa marehemu uligundulika baada ya mfanyakazi
mwenzake wa kiume kumpigia simu saa 2 asubuhi ambapo simu yake ilikuwa
ikiita bila kupokelewa ndipo alipoamua kwenda kumgongea katika chumba
hicho.
Alisema baada ya kufika alishangaa kukuta mlango wa chumba chake uko
wazi na alipochungulia alibaini kwamba Blandina alikuwa amefariki dunia.
Hata hivyo, polisi baada ya kufika na kuufanyia uchunguzi wa awali
mwili huo hawakugundua kuwepo kwa jeraha lolote linaloashiria kuuawa,
ingawa mwili huo ulipelekwa kufanyiwa uchunguzi wa kitaalam katika
Hospitali ya Mkoa ya Mount Meru.
Jeshi la Polisi mkoani Arusha limethibitisha kutokea kwa tukio hilo
na kusema kuwa mwili wa marehemu umehifadhiwa katika chumba cha
kuhifadhia maiti katika hospitali hiyo.
0 comments:
Chapisha Maoni