IKIWA imebaki siku chache kabla ya Galatasaray kuikaribisha Chelsea
katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa barani Ulaya, kumezuka vurugu za
kupigana na kurushiana viti kati ya mashabiki wa Galatasaray na mahasimu
wao Besiktas katika mitaa ya jiji la Istanbul.
Kumekuwa na picha za
video katika mtandao wa Youtube ukionyesha makundi makubwa ya wahuni wa
Galatasaray na Besiktas wakichapana katika mitaa yenye maduka mengi
kabla ya mchezo baina ya timu hizo katika Uwanja wa Turk Telekom.
Vurugu hizo ziliendelea pia wakati wa mchezo huo ambao Galatasaray ilishinda kwa bao 1-0. Mashabiki wa Chelsea watakaosafiri kwenda jijini Istanbul kwa ajili ya kuishangilia timu yao wameonywa kuwa makini pindi watakapokuwa huko.

0 comments:
Chapisha Maoni