Akizungumza na gazeti hili juzi jijini Dar es Salaam, mtoa habari ambaye
aliomba hifadhi ya jina alisema kuwa, Februari 17, mwaka huu, staa huyo
atatakiwa mahakamani hapo kwa ajili ya kesi yake kuanza huku akisema,
kuna mabadiliko kidogo katika kusikilizwa kwa kesi hiyo.
Kwa mujibu wa mtoa habari huyo, Lulu mwenye umri wa miaka 18, atasomewa upya mashitaka dhidi yake ambapo atatakiwa kujibu tena kama anakubali aliua bila kukusudia au la!
“Elizabeth (Lulu) atasomewa upya mashitaka ya kumuua Kanumba bila kukusudia.
“Ataulizwa ni kweli au si kweli? Atatakiwa kujibu swali moja kati ya hayo mawili, kama ni kweli atasema kweli kama si kweli atasema si kweli,” kilisema chanzo hicho huku kikisisitiza jina lake lisichorwe gazetini.
MUDA WA KESI SIKU 730
Habari zaidi zikadondokea Dawati la Risasi Jumamosi na kusema kwamba, kesi hiyo itaendeshwa kwa siku mia saba na thelathini (730), kwa maana ya miaka miwili hadi hukumu itakapotolewa.
NI NDANI YA SHERIA MPYA
Katika Siku ya Sheria Duniani iliyoadhimishwa jijini Dar es Salaam, Februari 3, mwaka huu, Jaji Mkuu wa Tanzania, Mohamed Chande Othman alisema kuanzia sasa kesi zote za jinai zitatakiwa kumalizika katika kipindi cha miaka miwili.
Kesi ya Lulu nayo ni ya jinai na kwa sababu hiyo, hadi Februari ya mwaka 2016 itatakiwa iwe imemalizika.

WAKILI WAKE
Chanzo hicho kililithibitishia gazeti hili kwamba, Lulu atatetewa na yuleyule wakili wake mwenye ‘ngekewa’ ya kuwatetea watu maarufu nchini, Peter Kibatala.

Kibatala ameshawahi kuwa wakili wa Mbongo Fleva, Isaac Waziri Makuto
‘Lord Eyez’ katika kesi ya madai ya kuiba ‘power window’ za gari la
msanii mwingine wa Bongo Fleva, Omary Faraji Nyembo ‘Ommy Dimpoz’.
Pia aliwahi kumwakilisha wakili mwezake, Mabere Nyaucho Marando
kwenye kesi ya Mbongo Fleva, Judith Wambura ‘Jide’ alipoburuzwa kortini
na uongozi wa Clouds Media Group baada ya Marando kuwa na udhuru.
Ilibaki kidogo awe wakili wa Miss Tanzania 2006, Wema Isaac Sepetu
katika kesi ya kumpiga makofi meneja wa hoteli moja (jina tunalo)
iliyopo Kawe Beach, Godluck Kuyumbu lakini akakosa sifa baada ya shauri
hilo kusiklizwa Mahakama ya Mwanzo Kawe, Dar.
HAWA HUENDA WAKAITWA
Kwa mujibu wa mtoa habari wetu, katika kesi hiyo huenda wakaitwa watu ambao watasaidia kutoa ushahidi.
Watu hao ni wale waliokuwa na ukaribu na marehemu, hasa siku ya tukio au kushirikishwa kwa namna moja au nyingine kwa jinsi ambavyo waendesha mashitaka wataona.
DOKTA KIDUME
Aliyekuwa akimtibu Kanumba, Dokta Kidume anaweza kufika mahakamani hapo kwa sababu ndiye aliyekuwa mtu wa pili kufika kwenye chumba cha marehemu mara baada ya kuanguka.

0 comments:
Chapisha Maoni