TIMU ya Arsenal FC imepokea kipigo cha bao
2-0 kutoka kwa Bayern Munich katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya
iliyochezwa Uwanja wa Emirates, London hivi punde.
Arsenal waliokuwa nyumbani katika Uwanja
wao wa Emirates wamemaliza mchezo wakiwa 10 baada ya kipa wao Wojciech
Szczesny kumchezea rafu wimba wa Bayern Munich, Arjen Robben aliyekuwa
anaelekea kufunga bao.
Baada ya rafu hiyo, Szczesny alizawadiwa kadi nyekundu na kuamriwa ipigwe penalti langoni mwa Arsenal japo David Alaba aliikosa.
Mechi ya leo imeshuhudia timu zote mbili zikikosa penalti ambapo ya Arsenal imekoswa na Mesut Ozil na ya Munich ikikoswa na David Alaba.
Wafungaji mabao ya Munich walikuwa Toni Kroos na Tomas Muller.



0 comments:
Chapisha Maoni