Zdravko Logarusic ‘Loga’, akipanga kuwapa
mazoezi maalum washambuliaji wa timu hiyo ili kuweza kuziona vema nyavu
za wapinzani wao, amesema hana wasiwasi kuhusu timu hiyo kutwaa ubingwa
wa Ligi Kuu Bara huku akieleza sehemu ya kuzipuku Yanga, Azam na Mbeya
City.
Huku akisifu safu yake ya ulinzi kwa kutoruhusu bao katika mechi yao
ya kwanza ya mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara iliyomalizika
kwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Rhino Rangers ya Tabora,
Loga alieleza kujawa na furaha kwa kuwa bado hajakutana na timu hizo
zilizopo juu yake katika msimamo wa ligi hiyo.
Akizungumza na gazeti hili jana jijini Dar es Salaam, kocha huyo raia
wa Croatia alisema wakati huu wakijiwinda dhidi ya JKT Oljoro Jumamosi
mechi itakayopigwa Uwanja wa Taifa, atabadilisha aina ya mazoezi ili
kutoruhusu hali ya kupoteza nafasi kama ilivyotokea katika mchezo
uliopita.
Lakini alifafanua kuwa anaamini bado nafasi ya kutwaa ubingwa wa ligi
kwa timu yake ipo kutokana na kwamba ana mechi na timu zote tatu
(Yanga, Azam na Mbeya City) na klabu hizo pia zikitakiwa kukutana
zenyewe kwa zenyewe jambo litakalobadili msimamo.
“Kama nitashinda mechi zote dhidi ya Yanga, Azam na Mbeya City, ni
wazi kuwa tutapanda kwenye msimamo, naamini ushindi kwa kila mechi ndiyo
utakaotoa mwangaza kabla ya kufika mwisho wa msimu,” aliongeza Loga.
Logarusic alisema pointi tatu na wingi wa mabao ni muhimu katika ligi
kwa sababu timu zote zilizoko chini kwenye msimamo wa ligi hiyo
zinakimbilia juu kwa sasa.
Kocha huyo alisema anaamini mechi dhidi ya JKT Oljoro itakuwa tofauti
zaidi kwa sababu tayari ameshagundua makosa yaliyofanywa na wachezaji
wake.
“Kila mechi unajifunza wapi kuna makosa na jukumu la mazoezini ni
kukumbushana nini kifanyike katika mechi inayokuja, natumai mechi ijayo
timu itakuwa bora na imezidi kuimarika,” aliongeza kocha huyo.
Alisema anahitaji kuwa na wachezaji wabunifu na wanaosikiliza
maelekezo yake kwani kwa kufanya hivyo timu itajiweka kwenye nafasi
nzuri ya kupata ushindi.
Alisisitiza nidhamu ya kiufundi kuanzia mazoezini hadi ndani ya mchezo ndiyo msingi na siri ya mafanikio.
Ligi Kuu ya Bara inatarajiwa kuendelea tena leo katika viwanja vinne
tofauti huku mechi inayoonekana kuwa na upinzani mkali ikiwa ni kati ya
mabingwa watetezi, Yanga itakayokuwa ugenini jijini Tanga kuwakabili
wenyeji Coastal Union kwenye Uwanja wa Mkwakwani.
Mechi nyingine zitakazopigwa leo ni kati ya Azam dhidi ya Rhino
Rangers (Azam Complex, Chamazi), Kagera Sugar dhidi ya Mtibwa Sugar
(Kaitaba, Bukoba) na Ruvu Shooting itaikaribisha Mbeya City kwenye
Uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani.
Yanga inaongoza msimamo wa ligi hiyo ikiwa na pointi 31 ikifuatiwa na
Azam na Mbeya City zenye pointi 30 kila moja huku Simba ikishika nafasi
ya nne ikiwa na pointi 27.
0 comments:
Chapisha Maoni