Rais wa Ukraine, Viktor Yanu-kovich, amekubali ombi la
kujiuzulu kwa waziri mkuu wa taifa hilo, Mykola Azrov, pamoja na baraza
zima la mawaziri licha ya hatua muhimu kupigwa mnamo Jumanne.
Hata hivyo mawaziri hao waliojiuzulu wanasalia kuwa wasimamizi wa wizara zao hadi pale serikali mpya itakapo buniwa.
Awali bunge la Ukrain lilipiga kura ya kuifutilia mbali sheria kali
dhidi ya maandamano ambayo ilizua ghasia tangu iidhinishwe mwezi
uliopita.
Kura ya kuifutilia mbali sheria hio ilipigwa na asilimia kubwa ya
wabunge wa taifa hilo. Sheria hio ilipiga marufuku waandamanaji kutumia
majengo ya umma pamoja na kuvaa vinyago.
Mwandishi wa BBC nchini Ukraine, amesema kuwa upinzani utaiona hatua
ya waziri mkuu kujiuzulu pamoja na kufutilia mbali sheria inayozuia
maandamano kama ushindi kwao
Mgogoro wa kisiasa nchini Ukraine, ulianza kama maandamano ya amani
mwezi Novemba wakati ambapo Rais Yanukovych alipokataa kutimiza ahadi
yake ya kushirikiana na Muungano wa Ulaya.
Waandamanaji hata hivyo wameapa kuendelea kuandamana hadi Rais Yanukovych atakapojiuzulu.
0 comments:
Chapisha Maoni