Alhamisi, Januari 09, 2014

RIPOTI KAMILI YA BASI LA MTEI KUCHOMWA MOTO JANA IKO HAPA

Huko Singida watu wenye hasira walilichoma moto basi la Kampuni ya Mtei Express ya mjini Arusha, baada ya kulituhumu kuhusika katika ajali ya kuigonga pikipiki na kuua watu watatu wa familia moja.
Watu hao ni Tamili Shaban na Kassimu ambao walifariki papo hapo kwenye eneo la tukio ambalo ni kitongoji cha Ijanuka kijiji cha Kisasida Manispaa ya Singida.Hamza amefariki dunia akiwa anaendelea kupatiwa matibabu katika hospitali ya mkoa mjini hapa. Miili ya watu hao imehifadhiwa.
Akizungumzia tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, SACP,Geof

rey Kamwela, alisema tukio hilo lililitokea jana saa moja na dakika moja asubuhi huko katika Kitongoji cha Ijanuka Kijiji cha Kisasida.
Alisema siku ya tukio, basi la Kampuni ya Mteni lenye namba za usajili T.742 ACU aina ya scania likiendeshwa na Dismas Ludovick, lilikuwa linatokea Singida mjini likielekea Arusha mjini.
Kamwela alisema lilipofika Kitongoji cha Ijanuka, pikipiki iliyokuwa inaendeshwa na Shaban Bunku huku akiwa amepakia watoto wake watatu, ilikatisha ghafla kitendo kilichosababisha kugongwa na kuburutwa kwa hatua 20.

0 comments:

Chapisha Maoni