Alhamisi, Januari 09, 2014

MTU MMOJA ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA BAADA YA KUKAMATWA NA VIPODOZI VILIVYO PIGWA MARUFUKU

Mnamo Tarehe 08.01.2014 Majira Ya Saa 16:30hrs Huko Ifisi, Kata Ya Utengule, Tarafa Ya Usongwe, Wilaya Ya Mbeya Vijijini, Mkoa Wa Mbeya, Askari Polisi Wakiwa Doria  Walimkamata Dastan  Gama, Miaka 38, Mngoni, Mfanyabiashara, Mkazi Wa Songea Akiwa Na Vipodozi Vilivyopigwa Marufuku Na Serikali. 
Vipodozi Hivyo Ni Sabuni Box 2, Carolight Ndogo Dazani 4, Epictem 10, Extra Crela Dazani 2, Diproson Dazani 17, Movey Dazani 4, Soft Touch Dazani 4, Na Lemovet Box 3. Mtuhumiwa Alikamatwa Baada Ya Ushirikiano Kati Ya Jeshi La Polisi Na Raia Mwema. Bidhaa Hizo Zilikutwa Zimefichwa Vichakani. 
 Taratibu Zinafanywa Ili Afikishwe Mahakamani. Kamanda Wa Polisi Mkoa Wa Mbeya Kamishna Msaidizi Mwandamizi Wa Polisi Ahmed Z. Msangi Anatoa Wito Kwa Jamii Kuendelea Kutoa Taarifa Za Mtu/Watu Wanaoingiza Na Kuuza Bidhaa Zilizopigwa Marufuku Pindi Wanapoona Viashiria Vya Watu Wanaojihusisha Na Biashara Hiyo Kwani Vipodozi Hivyo Vina Athari Za Kiafya Kwa Watumiaji.

0 comments:

Chapisha Maoni