Watu kadhaa wanahofiwa kupoteza maisha yao baada ya boti ya MV
Kilimanjaro 2 inayomilikwa na shirika la Azam Marine kukumbwa na dhoruba
katikati ya bahari, wakati ilipokuwa safarini kutoka kisiwani Pemba
kuelekea kisiwani Unguja.
Baadhi ya habari nchini Tanzania zimelinukuu jeshi la polisi likidai
kuwa, baadhi ya abiria waliokuwemo kwenye boti hiyo walichukua majaketi
ya kujiokolea na kuyatupa nje ya boti hiyo.
Hata hivyo watu mbalimbali waliokuwemo kwenye boti hiyo walipohojiwa
na vyombo vya habari wamesema kuwa majaketi yaliyokuwemo yalikuwa
hayatoshi na watu waliyapata kwa kugombania.
Hadi hivi sasa idadi hasa ya watu waliopoteza maisha yao
haijajulikana. Taarifa zinaongeza kuwa, boti hiyo ilikuwa na abiria 69
watu wazima, abiria watoto 60 na mabaharia wanane.
Iliondoka saa mbili asubuhi kisiwani Pemba kuelekea kisiwani Unguja,
na ilipofika katika eneo la Nungwi bahari ilichafuka na boti ikaanza
kuyumba.



0 comments:
Chapisha Maoni