Rehema Chalamila ‘Ray
C’ ambaye alitopea kwenye matumizi ya madawa ya kulevya kisha
kuyaacha, amefunguka kuwa yupo fiti na anataka kuishi na mpenzi, hayupo
tayari kuteseka.
Ray C alifunguka hayo kupitia kwenye ukurasa wake wa mtandao wa
Instagram hivi karibuni ambapo bila hiyana alishindwa kuzuia hisia zake
kama binadamu, akasema anatamani sana kupata mume anayempenda ili azae
naye watoto wawili.
Ray C ambaye hivi sasa yupo mstari wa mbele katika harakati za kupiga
vita madawa ya kulevya, alisema anatamani kuwa na mume kwa sababu
hataki familia ya mzazi mmoja kulea watoto kama alivyolelewa yeye na
mama pekee.
“Mimi nimelelewa na mama tu, malezi hayo siyo mazuri kabisa. Sipendi
yatokee kwa wanangu ndiyo maana natamani nimpate mtu ambaye ananipenda
kutoka moyoni, tufunge ndoa kabla ya kuzaa,” alisema Ray C.
Baada ya mwanamuziki huyo kuandika ujumbe huo mtandaoni, walijitokeza
wadau wengi ambao walikuwa wakimtakia baraka ili ndoto zake zikamilike
huku wengine wakijitokeza na kumwambia wako tayari kumuoa.




0 comments:
Chapisha Maoni