Rais Obama ametumia hotuba yake ya kila mwaka kwa
taifa kuelezea jinsi atakavyotumia madaraka yake kujaribu kuimarisha
uchumi wa marekani na pia kukabiliana na bunge la Congress ambalo
linashuhudia mgawanyiko.
Bwana Obama ameutaja mwaka 2014 kuwa mwaka wa
mafanikio kwa Marekani na kusema kuwa China sio tena mahali bora pa
kuekeza bali ni marekani.
''Haya ndiyo matokeo ya juhudi zenu: kupunguza kiwango cha ukosefu wa ajira kwa kiwango kikubwa zaidi katika kipindi cha miaka mitano. Sekta ya nyumba na makaazi iliyofufuka. Sekta ya utengenezaji bidhaa inayobuni nafasi za ajira kwa mara ya kwanza tangu miaka ya tisini. Mafuta zaidi yanazalishwa hapa nyumbani ikilinganishwa na yale tunayonunua-hili limetokea kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka ishirini. Nakisi katika bajeti yetu ilipungua kwa zaidi ya nusu. Na kwa mara ya kwanza katika kipindi cha zaidi ya mwongo mmoja, viongozi wa kibiashara kote duniani, wametangaza kuwa China haiongozi tena kama eneo bora la kuekeza duniani bali ni marekani,'' amesema rais Obama.

Kadhalika
bwana Obama amesema licha ya kushuhudia miaka minne ya ukuaji wa uchumi
na faida kubwa iliyovunwa na makampuni, ukosefu wa usawa umezidi kukita
mizizi nchini marekani.
Amesema ametoa mapendekezo ya kuimarisha ukuaji. Bwana Obama amesema:
''leo, baada ya ukuaji wa uchumi kwa kipindi cha
miaka minne, faida za makampuni ya bei ya hisa zimekuwa juu, na
zilizokuwa juu zimezidi kuwa bora. Lakini mishara ya wastani bado iko
palepale. Ukosefu wa usawa umezidi kukita mizizi.''
Kuhusu usumbufu wa bunge la Congress, bwana
Obama amesisitiza kuwa yuko tayari kuendelea kufanya kazi na wabunge wa
Congress kurekebisha baadhi ya mambo, lakini hatasita kutumia fursa
nyingi zitakazojitokeza kadri iwezekanavyo kuchukuwa hatua za
kurekebisha mambo hata bila marekebisho ya sheria kupitia Congress.
0 comments:
Chapisha Maoni