Jumatatu, Januari 27, 2014

NDESAMBURO AJIGAMBA KUWA CHADEMA ITACHUKUA MAJIMBO YOTE KILIMANJARO 2015

Mbunge wa Moshi Mjini, Philemon Ndesamburo alisema chama hicho kitatumia kila aina ya ‘silaha’ kilichonayo kuhakikisha majimbo yote ya Mkoa Kilimanjaro yananyakuliwa na chama hicho 2015.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Ndesamburo alisema hakuna kikwazo kuyatwaa majimbo hayo kwa vile CCM, kimeshindwa kuwaletea Watanzania maisha bora kama waliyojinadi mwaka 2010.
Kwa sasa Chadema kinashikilia majimbo ya Moshi Mjini kwa vipindi vitatu mfululizo (2000-2015), Jimbo la Hai na Jimbo la Rombo wakati Chama cha Mapinduzi (CCM) kikishikilia majimbo matano.
CCM kinashikilia majimbo ya Moshi Vijijini, Siha, Mwanga, Same Mashariki na Magharibi wakati Tanzania Labour Party (TLP), kikishikilia Jimbo la Vunjo kupitia Mbunge wake, Augustine Mrema.

0 comments:

Chapisha Maoni