MSANII wa Kundi la Kaole Sanaa, Zaina Ramadhan ‘Nandi’ anasumbuliwa na
ugonjwa wa mifupa akidai kuvunjika pingili za mgongo kisha kushindwa
kutembea na kufanya kazi zake za sanaa na nyinginezo.
Akipiga stori na mwandishi wetu hivi karibuni, Nandi alisema kuwa
alianza kuumwa baada ya kupata hitilafu mwaka 2012 alipokuwa akitoka
Chuo cha Sanaa pale Lego, Ubungo jijini Dar.
Nandi alisema siku ya tukio alikuwa akivuka barabara ambapo
alishangaa kuona mguu umesita ghafla akashindwa kutembea hadi watu
wakambeba kumsaidia kuvuka.
“Sikujua kilichonipata, nikaenda nyumbani wakanichua na mafuta ya
asili ambayo yalinisaidia kidogo lakini tatizo lilizidi kuwa kubwa.
Nikiwa nyumbani mama aliniomba nimsaidie kubeba vyombo lakini
nilishindwa kuinua beseni baada ya kuinama na pingili za mgongo
zikavunjika,” alisema Nandi.
Baada ya hapo, Nandi alisema alikwenda Hospitali ya Mwananyamala,
Kinondoni jijini Dar ambapo alimuona daktari akamuandikia dawa za
kutuliza maumivu na kumhamishia Muhimbili kwa uchunguzi zaidi.
“Hapa nilipo sina uwezo kabisa kwani dawa nilizoandikiwa zinauzwa
ghali sana, familia imejitahidi kunisaidia lakini bado, nawaomba
Watanzania wanisaidie ili nipate matibabu kwani sielewi tatizo langu ni
nini kutokana na kukosa vipimo,” alisema Nandi.
Nandi amewahi kucheza filamu mbalimbali ikiwemo Yatima, Jua la Kiama, Kuzaa si Kupata na nyingine nyingi.
0 comments:
Chapisha Maoni