Habari kutoka Cairo, mji mkuu wa Misri zinasema kuwa, takriban watu 5 wameuawa na zaidi ya 45 wamejeruhiwa kufuatia mlipuko mkubwa wa bomu uliotokea kwenye jengo linalotumika kama makao makuu ya polisi nchini humo.
Mlipuko wa mjini Cairo umetokea siku moja kabla ya maadhimisho ya mwaka wa pili tangu kutokea mapinduzi ya wananchi ya Januari 25 mwaka 2011 yaliyomuondoa madarakani dikteta wa zamani wa Misri, Hosni Mubarak. Usalama umeimarishwa na polisi imesema uchunguzi umeanzishwa kuhusiana na shambulio hilo.
0 comments:
Chapisha Maoni