NOMA sana! Baada ya kupigwa cha mbavu (kuachwa) na Beautiful Onyinye,
Wema Isaac Sepetu huku akimnyang’anya vitu vyote vya ofisini, yule
kigogo wa ikulu, Clement a.k.a CK, hivi sasa anadaiwa kutoka na shosti
wa staa huyo, Naima Shaa.
Kwa mujibu wa chanzo makini, Naima anatamba na kuwapiga vijembe wasichana wa mjini
kuwa anatoka na CK mwenye mkwanja mrefu (bado fedha hazijaisha).
“Nakwambia hatunywi maji, mtoto kadata kabisa hadi ameamua kujichora
‘tatuu’ ya jina la Clement kwenye bega lake la kulia. Inahusu?”
kilihoji chanzo chetu.
Mpashaji huyo alizidi kuweka wazi kuwa Naima ambaye ni mtoto wa
Mbunge wa Mafia, Abdulkarim Shaa (CCM) hivi sasa anaonekana na mdogo wa
CK huku wakiitana shemeji wa ukweli.
“Sasa hivi jamaa anajilia vyake mdogomdogo kwa mtoto Naima pale kati, naona ameamua kumalizia machungu ya Wema kwa Naima.
“Unaambiwa nyuma ya pazia stori ni kwamba anataka Wema aumie ndiyo
maana ameamua kubanjuka na Naima huku akijua kabisa kuwa ni marafiki.
“Unajua kama mtu akikuumiza kimapenzi, ukitembea na rafiki yake naye
anaumia vibaya mno. Kwani hukumbuki ilivyokuwa kwa Penny (Penniel
Mungilwa) alipochukuliwa na Diamond (Nasibu Abdul)? Ilikuwa ni ili
kumuumiza Wema na kweli walifanikiwa. Ndicho anachokifanya CK,”
kilitiririka chanzo hicho.
Chanzo hicho kiliweka wazi kuwa Naima ambaye mara nyingi haoni soni
kuonesha tatuu ya jina la Clement, amekuwa akijinadi kuwa yeye ndiye
mrithi halali wa Wema na kwa sasa kigogo huyo haoni wala hasikii kwake.
“Naima naye amedata kabisa na sidhani kama anaogopa Wema kujua kama yeye
ndiye hasa anatembea na kigogo huyo kwa kipindi hiki,” kilisema chanzo
hicho.
Baada ya kupata taarifa hizo, gazeti hili lilimtafuta Naima ili
kuthibitisha madai hayo ambapo alikiri kumfahamu CK lakini akadai watu
wanamsingizia.
Alipoulizwa kuhusu tatuu aliyochora yenye jina la Clement, Naima
alisema ameandika ‘Element’ na siyo ‘Clement’ (tazama picha, akili ya
kuambiwa changanya na yako).
“Yeleuuuwi...jamani watu wananisingizia. Hii tatuu niliyochora
nimandika jina Element na siyo Element (angalia maneno yanafafa! Moja
alikuwa anamaanisha Clement),” alisema Naima na kukata simu.
Baada ya kuwasiliana na Wema kwa njia simu na kumuuliza kuhusiana na
madai ya zilipendwa wake kulipiza kisasi kwa rafiki yake, Naima, alisema
kuwa habari hizo ameshazisikia lakini anasikitika kwa kuwa kigogo huyo
karuka majivu na kwenda kukanyaga moto.
Alisema kuwa ishu hiyo haimuumizi na zaidi sana anawaombea wawili hao
maisha mema ya kimapenzi ilimradi moyo wake umeshatua kwa umpendaye.
“Moyo wangu ulishatulia kwa nimpendaye, nawatakia maisha mema,” alisema Wema.
Uchunguzi wa gazeti ulibaini kuwa nyuma ya pazia la habari hii kuna mambo mengi ya namna CK na Naima walivyokutana.
“Ni Kinondoni pale Mwanamboka. Mke wa CK alikuwa na baa pale ambayo siku hizi imefungwa.
“Naima alikuwa ni mke wa mtoto wa Mwanamboka. Walikuwa wanakutana pale baa. Ndipo mambo yalikoanzia.
“Naima alikuwa ni mke wa mtoto wa Mwanamboka. Walikuwa wanakutana pale baa. Ndipo mambo yalikoanzia.
“Unajua hata Naima ameingia kwenye gogoro la kindoa na mumewe kwa
muda mrefu. Kisa ni huyo CK. Ona sasa wote wamekosa ndoa. Sinema
inaendelea,” kilimalizia chanzo chetu.
0 comments:
Chapisha Maoni