MNAMO TAREHE 14.09.2013 MAJIRA YA SAA 14:20HRS HUKO KITONGOJI CHA KISUNGU KIJIJI CHA UPENDO KATA YA MAMBA WILAYA YA CHUNYA MKOANI MBEYA ASKARI POLISI WAKIWA KATIKA MSAKO WALIMKAMATA FELISTA D/O ROMAN, MIAKA 36, MNYAMWANGA, MKULIMA NA MKAZI WA KIIJIJI CHA KISUNGU AKIWA NA POMBE YA MOSHI [GONGO] LITA 12 KATIKA DUMU LA LITA 20, MBINU ILIYOTUMIKA NI KUIFICHA NDANI YA NYUMBA YAKE. MTUHUMIWA NI MUUZAJI NA MTUMIAJI WA POMBE HIYO. MTUHUMIWA AMEKAMATWA NA TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA MARA MOJA TABIA YA KUTUMIA POMBE HARAMU YA MOSHI KWANI NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI NA NI KINYUME CHA SHERIA .
0 comments:
Chapisha Maoni