Alhamisi, Septemba 05, 2013

WATU 2 WAMEFARIKI DUNIA NA WENGINE 3 KUJERUHIWA VIBAYA KATIKA MATUKIO MAWILI YA AJALI TOFAUTI MKOANI MBEYA

Watu wawili wamefariki dunia na wengine watatu kujeruhiwa katika matukio mawili tofauti yaliyosababishwa na ajali za magari mkoani Mbeya jana katika wilaya ya Chunya na Rungwe.


Katika tukio la kwanza mtu mmoja amefariki dunia na wengine watatu kujeruhiwa katika ajali ya gari iliyotokea huko wilayani Chunya mkoani Mbeya katika kijiji cha Mapogoro barabara ya Chunya/Mapogolo jana majira ya saa 11:00 jioni baada ya gari walilokuwa wakisafiria kupinduka.

Taarifa zinaekeza kuwa gari lenye namba za usajili T.198 AGT aina ya Mitsubishi Fuso lililokuwa likiendeshwa na dereva aliyefahamika kwa jina la Fransis Mahange, 31, Mkinga na mkazi wa kijiji cha Kibaoni lilipinduka na kusababisha kifo cha Joshua Msukula, 28, Mlambya, Mkulima na mkazi wa kijiji cha Sinjili.

Aidha taarifa zimeendelea kusema kuwa watu waliojeruhiwa katika ajali hiyo ni pamoja na Tumaini Mwaikambo,30, Mnyakyusa, Mkulima na mkazi wa Kibaoni, Eliza Boniface, 34, Msafwa, mkulima na mkazi wa Sinjili na wa mwisho ni Joshua Sheria, 30,Msafwa, mkulima na mkazi wa Sinjili na wote wamelazwa katika hospitali ya wilaya ya wilaya ya Chunya mkoani Mbeya na chanzo cha ajali hiyo bado hakijafamika.

Katika tukio la pili mtu mmoja amefariki dunia baada ya kugongwa na gari alipokuwa akiendesha baiskeli katika kijiji cha Kibumbe-Kiwira wilayani Rungwe mkoani Mbeya jana majira ya saa 4:00asubuhi.

Habari zinasema kuwa ajali hiyo imetokea katika barabara ya Tukuyu/Mbeya wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya baada ya gari aina ya Scania lennye namba za usajili T.993 AUL lililokuwa likiendeshwa na dereva aliyefahamika kwa jina la Lusubilo Semi, 33, Mnyakyusa mkazi wa Tukuyu kumgonga mwendesha baiskeli aliyefahamika kwa jina la Philmon Ezekiel, 22, Mmalila, mkulima na mkazi wa kijiji cha Kibumbe na kufariki papo hapo.

Mwili wa marehemu umekwisha fanyiwa uchunguzi na daktari wa serikali na kukabidhiwa kwa ndugu tayari kwa mazishi. Dereva amekamatwa na taratibu zinafanyika ili afikishwe mahakamani lakini chanzo cha ajali bado hakijafahamika.

Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya Kamishna msaidizi wa jeshi la polisi Diwani Athumani amethibitisha kutokea kwa matukio hayo na ametoa wito kwa madereva kuwa makini watumiapo vyombo vya moto kwa kuzingatia sheria za usalama wa barabarani ili kuepusha ajali zinazoweza kuepukika.

0 comments:

Chapisha Maoni