Polisi nchini Urusi wamemzuilia daktari mmoja
mpasuaji kwa madai ya kuiba kifuko kilichokuwa na dawa ya kulevya ya
Heroin kutoka tumboni mwa mgonjwa.
Polisi katika eneo la Siberian walimtaka daktari
kumfanyia upasuaji mshukiwa ili waweze kunasa dawa hiyo ambayo mgonjwa
alikuwa ameimeza. Hata hivyo polisi waligundua kuwa seheme ya dawa hiyo
iliyotolewa tumboni mwa mshukiwa ilikuwa inakosekana
Maafisa wa utawala wanadai kuwa daktari huyo
alikuwa mlevi walipomkamata. Huenda akafungwa jela kwa miaka 15 ikiwa
atapatikana na hatia ya wizi wa dawa za kulevya.
0 comments:
Chapisha Maoni