Tokyo imekuwa ikisherehekea kuchaguliwa kuwa mwenyeji wa michezo ya Olimpiki ya mwaka wa 2020.
Mji mkuu wa Japan uliishinda kwa urahisi miji ya Istanbul na Madrid.
Tokyo ni mji wa tano ambao utakuwa umeandaa Olimpiki mara mbili.
Mwandishi wa BBC amesema kuwa mji huo
ulijitembeza vyema katika siku ya mwisho ya kampeni lakini piya
ulionekana kuwa thabiti kifedha na kiusalama
Waziri Mkuu wa Japan, Shinzo Abe, aliiambia
kamati ya Olimpiki, IOC, kwamba matatizo ya miyonzi ya nuklia katika
kinu cha nishati cha Fukushima hayataathiri michezo mjini Tokyo.
0 comments:
Chapisha Maoni