Jumapili, Septemba 08, 2013

BEEF KALI LINANUKIA KATI YA MENGI NA MUHONGO...CHANZO NI TWEET YA MENGI

Reginald Abraham Mengi, Mwenyekiti wa Kampuni za IPP ameandika ujumbe kwenye Twitter akimshutumu Waziri wa Nishati na Madini, Sospeter Muhongo, kwa kile anachodai kuzushiwa jambo.

Jambo lenyewe ni umiliki wa vitalu; vya kuchimba madini, kwamba ameshindwa kuviendeleza. Ujumbe huo usiokuwa na jina la Muhongo umesambaa mno kwenye mitandao ya jamii; JamiiForums, Wanabidii, Mabadiliko na kwingineko na tayari idadi kubwa ya watu wanachangia kaoni yao.
Katika maoni hayo, wengi wanamshuktumu Waziri Muhongo.
Huenda hii ikawa vita nyingine baina ya wizara na Mengi na huenda zaidi yakasikikika siku chache zijazo, endelea kufuatilia ukurasa huu wa Tajoa kujua zaidi.

0 comments:

Chapisha Maoni