Jumanne, Septemba 03, 2013

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI “PRESS RELEASE” TAREHE 02. 09. 2013.

                                            WILAYA YA MOMBA – MAUAJI. 

MNAMO TAREHE 01.09.2013 MAJIRA YA SAA 13:00HRS HUKO KATIKA KITUO CHA AFYA KAMSAMBA WILAYA YA MOMBA MKOA WA MBEYA. MTOTO AINES D/O JOSEPHAT ZAKARIA, MWENYE UMRI WA MIEZI MINNE, MNYAMWANGA, MKAZI WA IVUNA ALIFARIKI DUNIA WAKATI AKIENDELEA KUPATIWA MATIBABU KATIKA KITUO HICHO CHA AFYA. CHANZO NI BAADA YA MAMA YAKE MZAZI PRISCA D/O WILSON AKIWA NA MTOTO HUYO MGONGONI KUSUKUMWA NA STEVEN S/O CLETUS KISHA KUMGONGESHA MTOTO UKUTANI NA KUMSABABISHIA JERAHA KUBWA KICHWANI TAREHE 27.08.2013 MAJIRA YA SAA 20:00HRS. MTUHUMIWA ALIKIMBIA MARA BAADA YA TUKIO. MWILI WA MAREHEMU UMEFANYIWA UCHUNGUZI NA KUKABIDHIWA NDUGU KWA MAZISHI. KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI BARAKAEL MASAKI ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA JUU YA MAHALI ALIPO MTUHUMIWA AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE, VINGINEVYO AJISALIMISHE.

    
                     WILAYA YA  MBEYA MJINI – AJALI YA  GARI KUMDONDOSHA ABIRIA NA
                                                               KUSABABISHA KIFO
.
                                         
MNAMO TAREHE 01.09.2013 MAJIRA YA SAA 10:45HRS HUKO MABATINI BARABARA YA META/STENDI KUU JIJI NA MKOA WA MBEYA. GARI T.773 BNL AINA YA TOYOTA P/UP LIKIENDESHWA NA DEREVA DESTON S/O KABISSA, MIAKA 29,KYUSA,MKAZI WA SAE LILIMDONDOSHA ABIRIA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA MOJA LA OSCAR S/O ? MWENYE UMRI KATI YA MIAKA 30 – 35 NA KUMSABABISHIA KIFO CHAKE PAPO HAPO. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA. CHANZO KINACHUNGUZWA. DEREVA AMEKAMATWA TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI.KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI BARAKAEL MASAKI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.

                                                   [BARAKAEL MASAKI - ACP]

                              KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

0 comments:

Chapisha Maoni